Tulonge

Arusha:Aliyemuua Bilionea Erasto Msuya akamatwa

Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa akihojiwa na makachero.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.

“Tumewakamata watu wametupa mwanga mzuri na huyo mfanyabiashara ndiye aliyetoa fedha za kununua pikipiki na siku moja kabla ya tukio zilihifadhiwa nyumbani kwake,” alidokeza polisi mmoja.

Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo.

Pikipiki hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla ya tukio zikahifadhiwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo hadi siku iliyofuata ambapo aliwakabidhi wauaji na zote zimekamatwa.

Mahojiano kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi yamekuwa yakifanyika kwa siri na katika kituo cha polisi (jina tunalo) na kwamba mambo ni mazuri.

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 677

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Swedi on August 21, 2013 at 12:16

Hapo huenda key point ni "TANZANITE" tajiri na maskini wote wanakua na wakati mgumu either duniani au akhera. La msingi mungu ajaalie uwe kati kwa kati...

Comment by David Edson Mayanga on August 16, 2013 at 12:06

Damu ya nwanadamu huwa haimwagiki bule lazima itaondoka nawengi ,kwani adhabu ya kuuwa hutoa mwenyezi mungu tu nasio mtu mwingine . yani dunia ya leo bwana ukuwa tajili shida ukiwa masikini ndio kabisa shida sijajuwa .

Comment by Mama Malaika on August 15, 2013 at 20:21
Hapo chanzo chake ni kirefu, maana mtuhumiwa ni mfanya biashara tajiri wa madini ya Tanzanite pia.
Comment by Mjata Daffa on August 15, 2013 at 17:28

ukiwa tajiri tabu! ukiwa masikini tabu sijui uwe nani

Comment by ANGELA JULIUS on August 15, 2013 at 15:51

PESA NDO KILA KITU SUBIRINI MUONE MATOKEO NDO MTACHOKA

Comment by chaoga on August 15, 2013 at 11:15

HUKO ARUSHA WATU WAMEKAA KIKAZI ZAIDI....

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*