Tulonge

Arusha: Kilichojiri kwenye mazishi ya Billionea aliyepigwa risasi takribani 20

Hapa utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Maremu Erasto Msuya.

MIRERANI zikiwa ni siku takribani sita zimepita tangu mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliyefahamika kwa jina la Erasto Msuya kupigwa risasi zaidi ya ishirini na kufariki dunia papo hapo katika eneo la Bomang'ombe karibu na njia panda ya KIA (Kilimanjaro International Airport). Kifo hicho kilichokua na utata mkubwa na kupelekea watu wengi kujiuliza maswali mengi yasiokua na majibu. Leo ilikua ni siku ya mazishi ya mfanyabiashara huyo ambaye kutokana na kuwa alikua akiishi jijini Arusha maeneo ya kwa Iddi ilibidi jana jumatatu wafanye utaratibu wa kuuga mwili wa marehemu nyumbani kwake na leo jumanne kwenda kuzikwa Mirerani katika kijiji cha Kairo.

 

Msiba wa Erasto ulikua ni gumzo kubwa sana na watu wamekiri hawajawai kuona msiba kama huu maana kilichokua kikiwashangaza watu ni jeneza lililokua likifunguliwa kwa rimoti, na pia ni mazishi yaliyokua na watu wengi sana. Kila kona kulikua na minong'ono ambayo ilikuwa ikizungumzia utata wa kifo chake. Kamati ya maandalizi ya mazishi wakishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki walijitahidi sana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa maana haikuwa kazi rahisi kuweza kumudu kuhakikisha usalama wa wingi wa watu uliokuwepo katika mazishi ya Erasto.

Hii ndio nyumba ya milele ya bilionea Erasto Msuya ikiandaliwa.

Wakati unaingia nyumbani kwa bilionea Erasto Msuya hili ndio bango lililokua limewekwa.

Mchungaji Abeli Msuya na mkewe wakitoa sala mbele ya jeneza la marehemu.
Familia ya marehemu katika ibada ya kumwaga marehemu Erasto Msuya iliyofanyika Jumatatu huko Sakina Arusha

Chanzo: Kingjofa Blog

Views: 1578

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Swedi on August 21, 2013 at 14:24

Nadhani watakua wamefunga na AC humo kaburini kwake.. Alafu eti mtu unafika mahali hujui kama kahela kako katakufikisha mwisho mwezi ili kamshahara kaingie hahahahahah raha sana tz

Comment by Tulonge on August 15, 2013 at 12:49

Pia nimesikia alizikwa na cheni yenye thamani ya million 10.

Comment by Tulonge on August 15, 2013 at 12:39

Mama nimecheka hicho Christer alichokiandika. Kuwa wamehangaika kutengeneza jeneza la kufunguka kwa remote control wakati akishazikwa hakuna atakaye lifungua huko kaburini. Labda kama niwe nimemuelewa sivyo

Comment by Mama Malaika on August 15, 2013 at 12:36
Tulonge unacheka nini??
Christer usemayo ni kweli...
Comment by Tulonge on August 15, 2013 at 10:30

Christer umenichekesha, eti kaburini nani atalifungua.

Comment by Christer on August 15, 2013 at 10:04

Jeneza linafunguliwa kwa remote sasa huko kaburini nani atalifungua?.......mmmh jamani

Comment by David Edson Mayanga on August 15, 2013 at 0:17

PUMZIKA KWA AMANI MILELE NDG YETU ERASTO MSUYA

Comment by ANGELA JULIUS on August 14, 2013 at 7:59

Apumzike kwa amani.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*