Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo katika kata ya Ngusero mkoani Arusha aliyedhalilishwa na vijana wa jamii ya kifugaji kwa kuvuliwa nguo zote na kuachwa uchi wa mnyama na kisha kutandikwa viboko amesema atanunua bunduki na kuitumia kuua endapo Serikali haitachukua hatua.
Mchungaji huyo alifanyiwa udhalilishaji huo hivi karibuni baada ya kuwatahiri wanawe katika hospitali ya Kiteto, jambo ambalo vijana wa jamii hiyo walisema ni kosa kwa kwenda kinyume na mila na destruri ya kuwatahiri kimila, na hivyo kumvua nguo, kumchapa, kumpiga na kumjeruhi.
Mchungaji huyo anasema aliripoti shambulio hilo katika kituo cha polisi na amekuwa akifuatilia lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya vijana hao wala kuulinda usalama wake ikiwa ni pamoja na kuenedelea kupewa vitisho.
Add a Comment
chezea viboko wewe,hasira mpaka mchungaji anavaa gwanda
Naona Mchungaji uzalendo ulimshinda.Ikabidi auweke uchungaji pembeni kidogo akavaa moyo ya mfuasi wa Boko haram. Na atawatandika kweli
Nyie hamjui machungu ya kuvuliwa nguo na kuchapwa tena mtu mzima na heshima zako...Unaweza hata kwenda kwa kalumanzila aiseee..hahahahhaha
HUYU MCHUNGAJI SASA NATAKA KAMA VILE KUMFANANISHA NA SHEHE ILUNGA UBWABWA.
HUSSEIN NKENJE UMENENA KWELI KABISA
Ha haa haa haaa... Alfan, baada ya kulipiza kisasi bahati mbaya kabla hujatubu mauti inakukuta.
Pole mchungaji. Kisasi + Bunduki kwa mchungaji toka lini vikaendana?
Hahahahahaaa... alfan bhana!! Hahahaaaa
Sasa tatizo kutubu mahakamani husamehewi dhambi @ Alfan
Hao jamaa ni manunda kweli yaani wanamvua nguo mchungaji na kumchapa viboko?? Hata ingekuwa ni mimi ningeweka uchungaji pembeni aisee natafuta mmoja baada ya mwingine nawatandika risasi za magoti nikishamaliza naenda kutubu...teheteheteheteheteh
HUYU NI MWINGINE AU NI YULE WA MWAKA JUZI? SASA WEWE MCHUNGAJI UNAJICHANGANYA, BIBLIA GANI INASEMA ULIPE UBAYA KWA UBAYA?
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge