Kaka Beda Msimbe mmiliki wa blogu ya Lukwangule Entertaiment akiwa nje ya basi anasema, “Jamani nimekutana na basi lenye namba za kisasa muundo wa mwaka arobaini na saba. Nimeambiwa kwa wenyeji wa Songea ni kama alama vile. Hili basi unaweza kulipanda bila kuwa na fedha kuna kitabu maalumu unasaini ukirejea unaweza kulipa kwa fedha au hata kwa kuku. Likienda mjini ujuwe linaweza kubeba mbuzi, mbao, nakadhalika. Nililishika nikalizunguka likanikumbusha basi za MORETCO na KAMATA enzi hizo! Kitunze kidumu” Nenda lukwangule.blogspot.com ujionee picha zaidi.
Add a Comment
hii ngoma kama una nauli dusko usipande, hii kwetu basi likishakuwa namna hii tunaita nauli mara mbili. ila mmiliki wa hili bus inaonekana ni muislam safi... kulipa mpaka mwisho wa safari...
Hata bure sipandi. Unaweza ukapanda ukatoka na tetenasi
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge