Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.
“Suala la Bunge kurushwa ‘live’ halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?” alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.
Source:Nipashe Ijumaa
Add a Comment
Hivi Unaon akili ya nipe ipo sawa?
Tehe.. unajua ndugu yangu Dismas.. Watu wanakurupuka sana. Sasa kwa hili huyu jamaa kachemka sana! Na nikiangalia na ile Taarifa ya bunge kuhusu bunge kurushwa "LIVe" ndo nimechoka kabisaa... yani hawa jamaa ni BOnge la wasani.. hahahaa.. Nimesema, ukikusanya haya matukio unaweza toa Bonge la muvi.. hahahaaa
Hebu Dismas unafikira hiyo muvi ingechukua jina gani ? HAHAHAHAAA
Huyu naye kachemka kweli, angeongea sababu nyingine lkn siyo ya watu kuwa maofisini asubuhi. Inamaana Vituo vya TV vyote viache kurusha matangazo yao asubuhi na mchana sababu watu wote wanakua maofisini. Siku hizi watu wanaangalia TV hadi maofisini. Atoe sababu nyingine
© 2019 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge