Tulonge

Chavez: Venezuela imefanikiwa kutengeneza Drone ya kwanza nchini humo kwa msaada wa Iran.


Rais wa Venezuela Hugo Chavez amesema kwamba nchi yake kwa mara ya kwanza imefanikiwa kutengeneza ndege ya kwanza ya kivita isiyokuwa na rubani {-unmanned aerial vehicle (UAV)-},na imepewa jina hili:Arpia-001 (Harpy-001),na kazi hiyo imetimia kwa kushirikiana na wataalamu wa Iran kwa ajili ya kuimarisha nguvu ya kujihami ya Taifa hilo la Amerika ya Kusini.
Venezuela kwa sasa inazalisha ndege za kivita zisizokuwa na rubani(Drones) na inataka kuongeza nguvu yake ya kujihami na ya kijeshi,suala ambalo halina nia yoyote wala uhusiano wowote wa kufanya chochote dhidi ya mtu yeyote,alisema Rais Chavez kauli hiyo siku ya Jumatano.

Aliongeza kauli hii kwamba:Ndege za kijeshi zisizokuwa na Rubani(Drones) zinahitajika kwa matumizi ya kijeshi na kiraia,huku akibainisha kuwa ndege hizo aina ya UAV zimetengenezwa kwa njia ambayo zinaweza kutumika kwa ajili ya shughuli zisizokuwa za kijeshi.

Venezuela ni Nchi yenye uhuru na Taifa huru,na inaendeleza mipango yake ili kuinua uwezo wake wa kujihami ikishirikiana na Iran,Russia,na China.Alisema Rais Chavez.

Drone hiyo inaweza kufuta masafa ya  kilomita 100,sawa na (Maili 60),na inaweza kuruka peke yake pasina kuwa na rubani kwa muda wa dakika 90 na kufikia (kimo) urefu wa mita 3,000,sawa na miguu elfu tisa (9,000 feet). Hadi sasa tayari Venezuela imeshafanikiwa kutengeneza na kuzalisha ndege tatu za angani.

Washington Dc mara kadhaa imeonyesha wasiwasi wake kuhusiana na  kiasi cha ongezeko la mahusiano kati ya Tehran na Caracas.

Habari na Chalii_a.k.a_ILYA

Views: 1062

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Gratious Kimberly on June 17, 2012 at 14:15

kudaaaadeki, walifikiri tutakufa wajinga na maskini?  hapo chacha..tushawajulia ndo maana tunawabana beneti hadi uvunguni mwao....swaaaaaaaaaafi sana.

Muda si mrefu utazikuta drone Afrika zinakagua wale wnaotuibia mali asili....kwanza Iran rafiki wa Tz...ngoja nimbeep Ridhiwani anipigie nimpe ishu amwambie mshua!!

Iam happy...technology grows in 3rd world country(wanavyo tuiuta)...haaaaaaaaaaaaa

Comment by ILYA on June 16, 2012 at 23:20

Kaka G @, hiyo ni Drone yenyewe halisi ya kudondosha cheche kama zile zilizoshuhudiwa kwenye vita vya  chechnya,unaambiwa hii drone iliyotengenezwa mitaa hiyo ya Venezuela ni noma,inakwenda kwa kasi kuliko hata mwanga,hala ikiachia kombora haikosei target,ni drone yenye hasira kinoma.!!

Chavez mwenye kakubali wataalamu wa kiiran si mchezo na ndio maana akaamua kutangaza wazi wazi kuwa utengenezaji wa drone hiyo umetimia kupitia msaada wa wataalamu wa kiiran.

Comment by Gratious Kimberly on June 16, 2012 at 5:05

Mhhhhhh......ebu zoom picha na uniongezeee nyingine nipige makofi....sijaona vizuri hapo...isije ikawa ni drone ya kudondosha vyakula kwa wale waliozidiwa vitani hahahahaha

Comment by chaoga on June 15, 2012 at 18:38

si mchezo wababe wa nguvu za kijeshi wakae sawa....

Comment by ILYA on June 15, 2012 at 18:01

Jana, mida ya saa tano za asubuhi na dakika 20 na sekunde nne (11:20:04 am) nilikuwa najiuliza swali hili lifuatalo:

Ni lini nchi za Afrika zitaanza kufikiria kuzalisha na kutengeneza Drones kwa ajili ya kuhami na kulinda nchi zao dhidi ya Majeshi ya west,na mawakala ya kijeshi ya west,na drones za kijeshi za west.?!

Kisha nikajiuliza swali hili:

Iran imeshatoa Promise kuwa iko tayari kushea uwezo wake na teknolojia yake kwa mataifa mengine yatakayohitaji hasa wale washirika wake.na sasa inaonyesha kwa vitendo utekelezaji wa promise yake.Kwa nini mataifa mengine pande za Afrika zisishirikiane na Iran katika sekta hizo na wakati Iran ishaweka wazi kuwa iko tayari kugawana teknolojia yake na atakayehitaji,jambo ambalo linayafanya mataifa ya kibeberu yachukie kuona Iran inashea Teknolijia na mataifa mengine.?!

Iko wazi kwamba hakuna  taifa kati ya yale mataifa ya kibeberu linaloweza au lililokuwa tayari kugawana uwezo wa kijeshi na mataifa mengine kama Iran,yako tayari yakuuzie silaha za kijeshi na hata kukupa bure,lakini sio kukupa teknolojia au kukuuzia teknolojia iliyotumika kutengeneza silaha hizo!!.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*