CHAMA cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA), kimetangaza kuanza mgomo kwa ajili ya kupinga manyanyaso wanayofanyiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) wa kuzikamata bila utaratibu.
Akitangaza mgomo huo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Sabri Mabrouk, alisema wamechukua uamuzi huo baada ya SUMATRA kufanya operesheni ya kukamata wagari yao wakiwatumia walinzi shirikishi.
Alisema kuanzia Jumatatu wiki ijayo, watasitisha kutoa huduma ya kubeba abiria kutokana na Mamlaka hiyo kushindwa kutekeleza jukumu walilonalo kwa utaratibu unaokubalika.
“Kimsingi tumekelwa sana na tabia hii ya kutumia watu wa pembeni kukamata daladala wakati si watumishi wa SUMATRA ambao sisi tunawatambua na kusababisha kero kwa madereva,” alisema.
Amewataka SUMATRA kuacha kutumia utaratibu huo badala yake kama wanataka kuendesha oparesheni hiyo, waingie wenyewe barabarani kwa kufuata utaratibu na sheria walizojiwekea.
Bw. Mabrouk alisema hadi sasa, zaidi ya daladala 100 zimekamatwa katika msako huo ambao unaoendelea ambapo daladala nyingine zaidi ya 6,000 zimejiandaa kusitisha huduma.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Daladala (UWAMADAR), Bw. Shukuru Mlawa, alisema kitendo cha SUMATRA kutumia wakala katika operesheni hiyo ni wazi kuwa jukumu hilo wamelishindwa.
“Awali mamlaka hii ilitaja sehemu korofi kwa madereva wa daladala ambazo ni Uhuru, Gongolamboto, Mbagala na Kawawa lakini bado wameshindwa kutekeleza kazi ya kukamata badala yake imewaagiza watu wa pemebeni kama vishoka,” alisema.
Chanzo: http://majira-hall.blogspot.com
Add a Comment
Mmmmmmmmmmmh, no comment
THem damn fool! SUMATRA + WAMILIKI wa DALADALA.
sasa mambo ya kupigana vibao yanatoka wapi ?
hahahahahaaaa,huyo afande niaje??????
Nasema na ntaendelea kusema hii sumatra ni janga la kitaifa,hawajui nini wanachokifanya maana wao wanaacha kusimamia taaratibu na sheria zilizowekwa,badala yake wamekuwa askari wa usalama barabarani.
Hivi sumatra mnatowaje kibali kwa mmiliki wa daladala bovu na halina vigezo vya kuwepo barabarani, au mpaka liue .halafu kwanini mtumie vishoka ktk kazi zenu,nyinyi mmeshindwa nini? acheni kunyanyasa watu.
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge