Mbilinyi akiingia mahakamani akiongozana na Mwanasheria wake, Lissu (picha: Lukwangule Ent. blog)
MWENDESHA Mashitaka wa Serikali (DPP) leo asubui aliambulia patupu baada ya Hakimu wa Mahamaka ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Dodoma, kumwachia huru Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, (CHADEMA) ambaye alimfikisha kizimbani kujibu tuhuma za kumkashifu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupitia mitandao ya jamii.
Awali, Wakili wa Mbilinyi ambaye ni Mwanasheria na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Mb, CHADEMA), aliitaka mahakama ifutilie mbali shitaka alilofunguliwa mteja wake kwa kudai kuwa halina msingi wowote wa kisheria.
Baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na Mwanasheria wa Serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno, “mpumbavu” ni lugha ya matusi, ndipo Hakimu alipoamua kulifuta shitaka lililowasilishwa kwake na kumwambia DPP akatengeneze upya mashitaka yake kwani aliyoyapeleka yalikuwa na hitilafu kubwa.
Via: wavuti.com
Add a Comment
mhh no comment
Kwa kweli ninashangazwa na uwezo wa watendaji wa serikali juu ya mambo wanayoyafanya kwa kukurupuka bila ya kuchunguza kwa jambo husika,Hivi wewe ni DPP unaandaa mashtaka ambayo hayana nguvu ya kisheria na wala ushahidi wa kutosha,ni kweli watu wamekuwa wakitumia mitandao kinyume kabisa na taaratibu zilizowekwa na mamlaka.
Lkn tujiulize neno mpumbavu lina maana ipi kwa ufahamu wetu wa kiswahili na pia kisheria tunaweza kuliweka ktk upande upi kabla ujampeleka mtu mahakamani,maana tumekuwa tukiitana majina ya mpumbavu,mjinga,fala bila kutambua athari za maneno haya kwa yule anayeambiwa.
Kuna mwimbaji mmoja wa mashairi alisema kuwa Neno la kitoto,mtoto kumwambia mtoto mwenzie tunasema anakua, lkn Neno la kitoto ,mkubwa kumwambia mkubwa mwenzie tunasema ni tusi haifai
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge