Tulonge

Elizabeth Michael "Lulu" kuachiwa kwa dhamana

Dhamana ya msanii wa filamu Lulu inaendelea kusikilizwa katika mahakama kuu kanda ya Dar es salaam na mpaka sasa upande wa serikali mawakili wamesema hawana pingamizi na dhamana hiyo,


Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Mahakama kuu ya Tanzania imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael aka Lulu aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania.


Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwakuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April 7, 2012, huko Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.Kanumba alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwake Sinza. source mpekuzi.

Chanzo: audifacejackson.blogspot.com

Views: 1338

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by David Edson Mayanga on January 29, 2013 at 18:09

kamenona kweli sasa

Comment by green ngusa on January 29, 2013 at 15:42

Hivi Lulu nini umejifunza katika maisha.Mhubiri anasema kuna wakati wa furaha na wakati wa huzuni.Mwanzo ulitoka wakati wa furaha kisha umepita wakati wa shida na sasa unarudi wakati wa raha. Fanya yampendezayo Mungu usije rudi wakati mbaya kuliko uliotoka.Hata pengine usipate nafasi ya kujirekebisha. Hongera kwa dhamana.

 

 

 

Comment by Christer on January 29, 2013 at 14:21

Heheheheheheheheheheheeeeeeeeeeeeeeee @ Mgao, eti kuuza cv, hata cv anayo? anauza sura tu, ila karembo na sura yake inauzika, teheteheeeeee. Tatizo mmezidi ubahili nyie kina mgao hamtoi cards hizo

Comment by MGAO SIAMINI,P on January 29, 2013 at 13:54

@Christer, aje ATM yake na kila kitu atapata sema kale katataka kaendelee kuuza cv Dar watakazongazonga mpaka wakaumize.

Comment by Christer on January 29, 2013 at 12:34

@ Mgao ATM cards please. hataki longolongo, heeheheheheheheheeeeee.

Comment by MGAO SIAMINI,P on January 29, 2013 at 12:27

sister Christer mi nataka aje iringa huku nimfiche mapapalazi na ile midume mibazazi isimsumbue

Comment by Christer on January 29, 2013 at 12:23

Hahhahahahahahahahaaaaa sasa mnatoa namba za simu tu hazitamsaidia, mtoe ATM cards + password ili zimsaidie jamani nyie wanaume mbona hivyo lakini? hahahahaahahahahaaa. Dogo ww unajichekea tu ss ww unatoa msaada gani? unampa nn? au unapeleka posa?

Comment by MGAO SIAMINI,P on January 29, 2013 at 12:21

Aje sasa kwenye kipupwe aache mbembwe

Comment by Tulonge on January 28, 2013 at 21:55

Hahhhhaaa Kheri chizi wewe

Comment by Tulonge on January 28, 2013 at 21:25

Hahahaaa mkuu Davud umenifurahisha, yani umetoa na namba kabisa.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*