Tulonge

Gari lakamatwa likiwa limebeba maiti yenye dawa za kulevya

Kutoka Morogoro taarifa ni kwamba jeshi la polisi la mkoa huo limefanikiwa kukamata gari ndogo aina ya Spacio likiwa na mwili wa marehemu ambapo zoezi hilo limefanikiwa baada ya taarifa kutoka kwa wasamariawema.
Kamanda wa polisi mkoani mbeya Faustine Shilogile amesema walipata taarifa za kuwepo kwa gari hilo ambalo lilikuwa linatokea Mbeya kuelekea Dar.

Polisi wa mkoa wa Morogoro waliweka mtego kwenye kituo cha Mikumi hatimaye na kufanikiwa kukamata gari hilo likiwa na watu watatu,pipi saba za vitu vinavyosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya na mwili wa marehemu.

Mwili huo ulivyopelekwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi umekutwa na pipi nyingine kumi na saba tumboni na inasemekana mtu huyo alifariki akiwa Mbeya.

Pipi hizi zimetolewa tumboni na zinafanyiwa uchunguzi kujuikana ni kitu gani lakini shaka kubwa zinaweza kuwa ni dawa za kulevya na haikuweza kuthibitishwa kwasababu bado hazijapitia kwenye maabara kwa ajili ya kuzitambua ni dawa za aina gani.

Watu wote watatu ambapo wawili wanahusika na gari hilo na mmoja ni mfanyabiashara wa Kariakoo wanashikiliwa na polisi huko Morogoro.

Via: mdodosaji blog

Views: 381

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*