Tulonge

Grace Mbowe dada wa Freeman Mbowe ajiunga CCM, awapa kadi ya CHADEMA

DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.


Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia.

Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.

Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai CHADEMA wanafanya propaganda zaAlisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka CHADEMA, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.

“Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.

Alisema, “kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”

“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga kushoto akimkabidhi yadi ya CCM, Grace Mbowe, baada ya kutoka CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.

Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.

Awali, akipokea kadi ya CHADEMA, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.

Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.

Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali CHADEMA ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.

Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea.

Via: HabariLeo

Views: 530

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mjata Daffa on August 30, 2013 at 9:40

Thank you for your understand Mgao

Comment by MGAO SIAMINI,P on August 29, 2013 at 21:48

@mjata nakuelewa ila nachomaanisha hana athari huyu mama sio ccm wala chadema uroho wake tu

Comment by Mama Malaika on August 28, 2013 at 14:54
Na huyu Grace Mbowe subirini, muda si mrefu utasikia kapewa uwenyekiti wa mkoa/wilaya au sehemu nyingine nzuri ya juu humo CCM au sirikalini.. Hiyo ndio siasa.....
Comment by Mjata Daffa on August 28, 2013 at 9:57

Kama utangulizi wangu ulivyotabiri nijua kwa hili tutatofautiana ndio maana nilitoa tahadhali, kwani kaka MGAO unadhani mm sijui process ya kusajili chama? huenda najua zaidi yako nininachosema hapa ni kuhusu rafu zinazochezwa na vyama vya siasa kuingiza mamluki kwenye vyama pinzani. nadhani mama malaika yeye amenielewa zaidi ndio maana akatoa mfano wa makongoro. unafahamu makongoro leo ni M/kiti wa CCM Musoma? je huoni aliend NCCR kufanya kazi maalum? usiitazame siasa kijuujuu siasa ni zaidi ya unayoyaona kwenye mgazeti.

Comment by MGAO SIAMINI,P on August 27, 2013 at 22:19

@mjata chama kinanza kichwani kwa mtu mmoja,wawili, watatu,nk kikianza sehemu au mtu fulani haina maana chake kusajiliwa kwake kwanza nilazima kikusanye wajumbe 200 kila mkoa wa tanzania chadema ni ya mamilioni sasa labda hufuatilii siasa za bongo ni tishio

Comment by Mama Malaika on August 27, 2013 at 12:15
Hii yanikumbusha Makongoro Nyerere. Mbio za 2015 zinaendelea hadi mwanzoni mwa 2015 tutasikia wengi na mengi. Siasa imetiwaliwa na pesa, iwapo wangekuwa wana siasa wanafanya kazi bila malipo na bila vyeo basi haya yangekuwa nadra sana
Comment by Mjata Daffa on August 27, 2013 at 9:29

wasadau kama siasa hatuifahamu naomba tusikomenti juu ya mada hii naogopa tusijetofautiana ni vigumu kuamini lakini cc wakongwe wa siasa tumekwishaliona hilo.

huyu Dada wa Mbowe amekwenda ccm kwa kazi moja tu, yakusafisha ile dhana ya chadema ni chama cha ukabila na familia ya mbowe.hana jipya muangalie alivyo anaonekana kabisa ametumwa kutoka DAR na CCM wameingia kichwakichwa kusapoti M4C. 

Comment by MGAO SIAMINI,P on August 27, 2013 at 9:13

kama haoni mabadiliko yoyote na wasiwasi na anachotumia kuangalilia kama anangalia kwa jicho la ccm ndo maana haoni. Atoke tu yeye ni mmoja tu na sisi tunapokea maelfu ya watu kila siku halafu chama sio cha familia ya mbowe mdogo wake ni mwenyekiti tu chama ni cha wananchi.

Comment by ANGELA JULIUS on August 27, 2013 at 7:06

NATUMAI MBOWE ATATOA TAMKO LOL.

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*