Tulonge

Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.

Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.

“Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii.

“Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali,” alisema Profesa Lekule.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.

Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.

Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.

“Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika,” alibainisha Profesa Lekule

Via: Jamii Forum

Views: 2119

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by CHA the Optimist on February 3, 2014 at 18:25

Wapi Mjata Daffa, wapi Zainabu Hamis?????

Comment by Mama Malaika on January 30, 2014 at 11:55
Dixon.... Asante sana kwa kunisamehe. Uliposema "PROF flani kakurupuka" wala hujakosea. Ha haa haa..

Kusema ukweli usalama kwenye chakula mdogo sana, hebu fikiria GM foods (Genetically Modified foods). The influence of Genetically Modified technology kwenye food supply chain inatisha. Tunashindilia na kula vyakula vyenye "modified genes and hormones" ambavyo vina madhara makubwa mwilini iwe kuku wa kizungu, sijui unga wa sembe ulio sagwa toka mbegu za misaada za Bill Gates kutoka Monsanto (genetically modified seeds) au zile Soya toka Monsanto.

Ni hatari tupu.
Comment by Dixon Kaishozi on January 30, 2014 at 8:32

Asante sana Mama Malaika.. Unajua kupotea kwako tunaweza kosa mengi.. Sasa nimekusamehe kutokana na kutujuza haya yote. Tunatofautiana uelewa ndiyo maana mi niliposema PROf. flan kakurupuka sikueleweka.. hehehehe

Kwa anae endelea kubisha na abishe, na anae jiona amepona kwa kutokula kitimoto aendelee na msimamowake huo huo!!! Ila kwa kifupi hajakwepa kitu..  Kama kaka Cha the Omniscient anavyotueleza na kurudia tena.. Utakwepa hapa... utapigwa pale.. 

Kwa ujumla tupo hapa kuelimishana, kujuzana, kufurahi na utani pia!! Sote tu familia moja ya wana TULONGE...

Pamoja sana!!!

Comment by Mama Malaika on January 29, 2014 at 19:46
Cha the Omniscient, nimekupata. Baadhi yetu hatukuzaliwa na kukulia kwenye tamaduni yenye mazingira ya kudadisi. Tunaburuzwa tu, iwe kushoto kulia tupo. Teh teh teh...

Mie si mlaji sana wa nyama (meat in general) ila nitagusia kidogo kwenye blog hii kuhusu maandiko matakatifu kwani kuna muingiliano (Jewish Law, etc.). Kwenye Bible, baadhi ya vitabu (Gospels) vimeandikwa under the influence of Jewish Law or Gentiles wa kipindi hicho. Mfano, lengo la kukataza ulaji wa nguruwe ilikuwa ni part of the ceremonial laws of the Old Covenant. Hivyo waweza jikuta unamaliza mwaka mzima kujiuliza kwa nini Mungu alipomuumba binadamu alimpa mamlaka (Genesis 9:2–4) kwa vile vitembeavyo nchi kavu na majini? Hivyo tunaposoma argument kwenye Gospels ina pasa ku digest na kujua ime base pande ipi.

Maandiko "The New Testament" imeandikwa kutokea tafsiri ya Coptic kwenda Greek, na baadae Greek kwenda Latin. Na wa Latin nao wakaichengenua Bible na kuacha baadhi ya Gospels na matokeo yake ndio kukazaliwa hii "The New Testament". Na ukiacha lugha hizo zilizopitiwa kupata hii "The New Testament", kanisa huko mwanzo (the Church Council) iliyoteuliwa kutafsiri (from Greek to Latin) ilichengenua na kuacha baadhi ya vitabu vingi toka kwenye "The Original New Testament" ikiwemo The Gospels of Thomas, John and Mary (mama yake Yesu). Na vitabu hivyo vyote vikawekwa kwenye list ya "Forbidden Books" kipindi hicho (in early Christianity).
Mfalme James (King James) aliyetawala Uingereza miaka ya 1600 na kitu (karibu miaka 400 iliyopita) naye akaandika (tafsiri) Bible yake from Latin to English na kuhalalisha itumiwe na Church of England pia itumike na wa Protestant duniani kote na ndio inayosomwa sasa. Na baada ya hapo ndio kukatokea mfumuko wa makanisa ya Evangelical (Sabato, Church of Christ na bado yanaendelea kila kukicha). Na sababu hiyo sishangai kuona makanisa yanatofautiana mara wale wana kula nguruwe, wale wanabatiza mtoto akiwa mdogo wengine wanasubiria akiwa kijana.
Nimebahatika kuisoma kidogo "The Original New Testament" toka Coptic Version unatakiwa uwe na moyo wa kutosha ku digest. Na haipatikani kirahisi kama Bible hii tuliyonayo. Hivyo mara nyingi nimekuwa makini sana kutumia Bible kwenye mijadala sababu ya hizi doctrines na pia influences kama vile Jewish Law zilizoko kwenye Bible. Na kitu kikubwa zaidi ni tafsiri (lost in translation), na ndio maana Gospels zilizotolewa kwenye Coptic version (origin) zinatofautiana na kwenye Bible ya sasa inayotumiwa. Baadhi ya maneno yalipohamishwa hamishwa na kipelekwa lugha hizo tofauti yamepoteza maana. Hata "The Old Testament" nayo hivyo hivyo kwani imetoka Hebrew Bible (ya wayahudi) ambayo iliandikwa kabla ya Yesu.

Ni hayo tu, samahanini kwa gazeti refu
Comment by CHA the Optimist on January 29, 2014 at 16:31
Omary acha mbwembwe bwanaaaa! unavyoitaja Rombo, Shitimbi, Butimba, Mikindani, Kishimundu, Tandahimba, Nakapanya, Sumbawanga, Daredi, Kateshi, utafikiri ulishafika...ha ha ha ha!
Comment by CHA the Optimist on January 29, 2014 at 16:15

Maisha yamejaa hatari za kila aina--ni ngumu sana kuzikwepa. Unaweza kukwepa mbele, nyuma unakutana nayo, waweza kukwepa kushoto, kulia unakutana nayo, waweza kukwepa chini, juu unakutana nayo. Ni ngumu sana, na kwa bahati mbaya yale ya uongo yamegeuzwa kuwa ya ukweli na ya ukweli yamegeuzwa kuwa ya uongo.

Comment by Mama Malaika on January 29, 2014 at 16:08
Nimepotea kidogo kwenye Tulonge kumbe napitwa mengi. Lol....
Every flesh (fat & muscle of an animal) tunayotia mdomoni ina bacteria, haijalishi iwe pork, beef, mutton, chicken, fish, bird, etc. Na ndio maana kwenye Food Hygiene tuna shauriwa nyama ipikwe na kuiva kabla ya kuliwa la sivyo waweza umwa. Na papo hapo tunaambiwa kuwa kuna bacteria kwenye vyakula hata ukichemshahawfi. Mfano wadudu walioko kwenye ya ng'ambo wanao sababisha ugonjwa wa BSE na CJD hata nyama ichemshwe vipi hawafi hata nyama ipikwe kwenye high temp bado bacteria hawafi, na yasemekana hata wakichomwa na radiation (mionzi) pia hawafi.

Dixon.... Magonjwa yako kila kona. Hata watu wakiacha kitimoto bado hayo maziwa ya ng'ombe nayo vile vile yabeba vidudu vya TB (tuberculosis) ndio maana kwa wenzetu mwiko kunywa maziwa yaliyokamuliwa toka kwa ng'ombe hadi yachemshwe kwenye machines with high temp na kuenguliwa (Pasteurization process) ndio wapewa unywe.
Ukiacha TB, maziwa na nyama ya ng'ombe wakati mwingine vinabeba BSE (Waingereza wanaita "Mad Cow Disease), ingawa nyama ndio source kubwa ya BSE, ni ugonjwa hatari sana unadhoofisha "Central Nervous System" na kuathiri mwili wote, na hauna tiba, una kufa na kuzikwa. Pia kuna CJD toka kwenye nyama ng'ombe hii ina dhoofisha ubongo na kufanya uwe msahaulifu na kuishia kuwa punguani, na ugonjwa hauna dawa.
Hapa UK, nyama ya ng'ombe lazima ipite sehemu tofauti kupimwa TMA special machines kuona kama imebeba vidudu vya CJD, BSE, etc. Na iwapo nyama itakutwa na vidudu basi yachomwa na authority wanakuja choma mifugo yako yote.
Ni kuomba Mungu atuepushe na majanga
Comment by Dixon Kaishozi on January 29, 2014 at 11:38

Kaka Omari umefafanua vizuri sana na kutoa mistari iliyokwenda shule kabisa. Big up!!! Sasa hapo tumetoka kwenye uprofesa na tafiti zao tumerudi kwenye maandiko matakatifu yanavyotuelekeza!!

Na kwa hiyo mistari uliyotoa.. Naamini majibu yamepatikana.. na anaye dhani kwamba kitimoto pekee ndiyo kimekatazwa na kukinyooshea kidole wakati anakandamiza vingine vilivyo kwenye hii mistari ni sawa na yule anaye kandamiza kitimoto kwa kwenda mbele!!!

Pamojah sana!!

Comment by Omary on January 29, 2014 at 10:05

 CHA the Omniscient Achana na kizungu sisi tumetoka kijijini sitimbi kishimundu, rombo  hatujui kidhungu unatuchangnya bhana soma maandiko hayo hapo nilioyatowa kwa lugha tunayoielewa kisha kama kuna swali naomba murudi kwangu kama hamjatosheka.

Comment by Omary on January 29, 2014 at 9:58

Acheni kubishana naomba kila mmoja ashike bible yake kisha asome Kumbu kumbu la Torati 14:3-6 wanyama walioruhusiwa kula,

7-8 wasioruhusiwa.

9 Samaki wa kuliwa
10 samaki wasioliwa

11 ndege wa kula

12-18 ndege wamekatazwa

19 watambaa


Pia ktk kitabu cha Mambo ya Walawi 11:13-23

KUMB 14:9-20 SAMAKI NDEGE WALIORUHUSIWA

Someni hayo mwenye swali aulize mimi nina Bible na Msahafu Mungu kasema mambo yote yatapita ila nena la Mungu halitabadilika hata  helufi 1 sasa ole wao wale walioichakachuwa bible wakahalalisha wayajuwayo wao mie simo ni yeye na Mungu wake.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*