Jamani napenda kuchukua fursa hii ili tuweze kuelimishana kuhusu unywaji wa pombe kwa kina mama wajawazito. Jambo hili limekua likitokea sehemu nyingi Duniani ikiwemo nchi yetu Tanzania. Najua hapa tulonge kuna kina mama wengi tu pamoja na madaktari (kama wapo) ambao wanaweza kutupa elimu juu ya hili.
-Je kuna madhara yoyote ambayo mama na kiumbe kilichopo tumboni wanaweza yapata?
Add a Comment
Ebwana ee:!! Doctor Fridolin@ asante sana umenikuna kwa ibara za kitaalamu za kibaolojia!Nimekubali sana comment hiyo ina mwanga zaidi.
Sasa mtoto si atalewa akiwa humo humo tumboni!!!,na akizaliwa ndio anakuwa mlevi kabisa!! wakati mwingine mtoto anaweza kurithi tabia za mama yake,ikiwa ni nzuri mtoto arithi na ikiwa ni mbaya anazirithi kwa wingi zaidi akiwa tumboni.
jamani hiyo labda sio pombe labda togwa hilo,,,,
hapo@ mama malaika mimi namshangaa na huo mchupa, mimi kinachonijulishaga ni mjamzito kabla hata sijafika kwa daktari ni kutapika pindi ninywapo pombe hasw zile siku za kwanza, hata iwe robo glass natapika hadi tone la mwisho.
Huyo mwanamke mwenzangu hapo juu pichani na huo mchupa sijui anamudu vipi hasa asubuhi akiamka sipati picha kwani mjamzito mara nyingi unakuwa dehydrated, sasa na hiyo hang-over ya pombe si ndio balaa?
Hapa naona watu wengi mmeongelea athari upande wa kiumbe (foetus) na sio athari kwa mama mjamzito ambaye kabeba huyo kiumbe.
Ushauri kuhusu pombe kwa wajawazito inategemeana nchi na nchi. Mfano hapa UK, nakumbuka mie nilipokuwa mjamzito mara zote, ile siku ya kwanza midwife anipatia kiji leaflet (Guidelines Advise from Health Department-NHS), moja ya vitu vilivyoandikwa humo ndani ni kwamba alcohol ni mbaya kwangu mama mjamzito na pili ni mbaya kwa kiumbe nilichokibeba tumboni, hivyo mama mjamzito sishauri kabisa kugusa/kunywa pombe kipindi chote cha ujauzito hadi hapo nitapojifungua.
Wakati hapa England hatushauriwi kabisa wajamzito kunywa pombe hadi hapo unapojifungua, Canada wao wanasema mama mjamzito aweza kunywa alcohol isiyozidi nusu ya unit moja (0.5 unit) kipindi chote hata iwe miezi 3 ya mwanzo kwani pombe nusu unit haiathiri foetus development kipindi cha mwanzo.
Mie kama mwanamke niliyebeba mimba na kuzaa, sishauri mjamzito anywe ili kujiweka kwenye nafasi nzuri hasa unaposumbuliwa na viji-magonjwa/matatizo vinavyojitokeza kipindi chote cha ujauzito kuanzia mwanzo hadi dakika ile unapoingia labour kama vile BP, sugar level, headache, .......
Kimtazamo wangu me kama me mwanamke mjamzito hatakiwi kunywa pombe kwani hicho kipimo ndio kazi na kama ujuavyo kitungi kikikolea hakuna kipimo wala nini pia haipendezi kwa mwanamke kunywa pombe kwani ikimkolea atakosa muda wa kuangalia watoto au watoto watajifunza nini? kutoka kwa mama jamani turudi kwenye IMANI zetu zinasemaje? hapa kwenye IMANI inagusa kotekote hina mwanamke wala mwanaume pombe ni KHARAM.
Asanteni wadau kwa elimu mliyo itoa. Doctor Fridolin asante kwa mchango wako wa kitaalam.
kaka @dick ant @manka na ancle @fridolin asanteni sanasana kwa elimu naamini mke wangu akipata mimba nitamsiklizisha mwanangu kawimbo ka R . L, au kumuimbia kawimbo ka kumbembeleza, kama kaka yangu dicked wakati alipokuwa anambembeleza kelvin akiwa katika katumbo ka mama yake, shukran kaka dicked kwa kaelimu,
ulevi na utumiaji wa pombe ka kweli ni vitu ambavyo kiutaalamu havitakiwa kutumika hasahasa wakati wa miezi mitatu ya kwanza" 1st trimester" wakati viuongo vingi vinatengenezwa," organogenesis", lakini pombe kiasi SI SANA, mtu anaweza kutumia baada ya miezi mitatu, yaan from second trimester. Lakini kwa ujumla hatushauri wajawazito watumie pombe
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge