Tulonge

Historia Fupi ya Mto Frati (Euphrates River)

Miongoni mwa mito ya zamani sana kihistoria ya enzi hizoooo,na ambao umebahatika kujizolea sifa kibao za kihistoria kutokana na Umuhimu wake hapa duniani ni Mto unaoitwa kwa kimombo:

Euphrates,au Al-Furat kwa Kiarabu,au Furat kwa Kituruki, au Frati kwa Lugha safi ya Kiswahili.

Mto huu ni Moja ya mito iliyokuwa muhumi sana katika Ulimwengu huu.Na hii ni kutoka (kama nilivyoashiria hapo juu) na umuhimu mkubwa uliokuwa nao mto huu kulingana na eneo ulipojiseti kijiografia.

Umekuwa siku zote ukitoa huduma pana ya maji kwa maeneo yote bali kwa nchi zote zinazopakana na mto huo.Mto huu uko nchini Iraq na sehemu ndogo ya Mto huu inaingia au inazihusisha nchi baadhi ambazo hupakana na nchi Ya Ira kama Uturuki na Syria.

Mto huu umekuwa ni chanzo cha msuguoano wa kisiasa,kwa sababu Uturuki,Syria,na Iraq wote kwa pamoja hushindana kwa ajili ya matumizi ya maji ya mto huu katika shughuli zao za kilimo hasa kwa umwagiliaji na uzalishaji nguvu za umeme kama wanavysoema kwa Lugha ya Kitaalamu"Generation of Hydroelectric Power".

Makarne kadhaa yaliyopita upande wa Mashariki wa Mto huu wa Frati ulikuwa chini ya Uthibiti wa Roma (au Warumi) ambao Dola lao wakati huo lilikuwa ni Dola lenye nguvu ambalo lilikiitwa "Roman Empire".

Ukiwa Kaskazini kwa Iraq Mto huu wa Euphrates utauona ukipakana na mipaka ya Magharibi ya eneo linaloitwa Al-Jazirah.

Mto huu ukiwa nchini Iraq utaukuta katika Jiji la Baghdad, a.k.a Jiji la milipuko. Kusini mwa Mji wa Baghdad ndiko kunapopatikana Mji wa Babylon,mji ambao naweza kusema ndio unaofaidika kwa kiasi kikubwa na maji ya Mto huu wa Frati.

Mto huu ni miongoni mwa mito iliyobahatika sana kupokea wageni wa Kitalii wanaokuja kutoka kila kona ya dunia ili kuutembelea na kuutizama ulivyoumbwa na aliyeuumba.

Lakini pamoja na hayo yote bado mpaka sasa Mto huu haujabahatika kutembelewa na mimi.


Na Chalii_a.k.a_ILYA

Views: 1446

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on January 31, 2012 at 22:43

Tena naiona Aswan hapo juu kwenye ramani yako, iko pembeni mwa mto Nile. Siku moja jaribu usafiri na Egypt Air halafu omba transit visa ingalau ukae siku 4 hadi week nchini Egypty na jaribu tembelea the Nile hadi kusini mwa Egypt, na sio utembelee middle east tu peke yake.

Comment by Mama Malaika on January 31, 2012 at 22:33

Ha haa haa haaa.... IL-YA, waarabu hawawezi kukubali kwani wanajisikia inferiors. Na sio wao tu hata wazungu nao ni hivyo hivyo ingawa sasa waingereza wameanza kuandika history yao upya na kukubali kuwa ni kweli kisiwa cha Uingereza kiliwahi kutawaliwa na mtu mweusi karibu miaka 1,800 iliyopita naye alikuwa ni Roman Emperor tokea Rome aliyehamishia makazi yake mji wa York ulioko Uingereza kaskazini, alifia hapo hapo mji wa York na kuzikwa hapo hapo. Ungekuwepo jirani yangu ningekuwa nakuazima hadi na vitabu.

Hao wote uliowataja wamo kwenye vitabu, Wawat walikuwa maeneo ya kusini mwa Aswan kwenye bonde la mto Nile. Mie mwenzio nilishafika Egypt hadi Abu Sembel Temples kutokea Cairo through the Nile kwa boat za kitalii. Hayo majengo ya Abu Sembel ukiyaona jinsi yalivyosimama hiyo milingoti (beam) ni mirefu hadi unajiuliza mwanadamu aliwezaje kulisimamisha mjiwe wote huo. Ni maajabu libakia mdomo wazi, hasa ukizingatia miaka hiyo hakukuwa na winch za kunyanyua lijiwe moja lenye matani ya uzito. Kipindi hicho Ulaya walikuwa na vijumba vya nyasi wakati Africa walikuwa na majumba makubwa makubwa huko Egypt. Ama kweli Black Civilization ni ya kuheshimiwa sanaaaa

Comment by ILYA on January 31, 2012 at 22:13

Eddie ngumi sirushi mbele mama Mkwe wewe sahau , unataka nikose mke,hahahaahah.

Mkwe kweli lazima tufaidike na Blog zenye faida kama hizi.Maana tunajifunza mengi na kujuzana mengi.Yani mkwe ungekuwa hapa ningefaidi sana kwa kuchukua maelimu kibao unayoyamiliki hasa hasa History,mtu mwenye ninavyopenda History sijui kama ungepumua mkwe au kumeza mate,hahaahahah.

Comment by ILYA on January 31, 2012 at 22:04

Mkwe yani kwa maelezo yako haya umegonha mle mle,niliwahi kusoma kitu ya namna hii kuhusu hawa wakushi kwamba ndio watu asili wa Iran,inagwa wairan ni vigumu sna kukukubalia.

Lakini ukweli ni kama unavyosema mkwe historia imethibitisha hilo.Nilisoma kitu hii lakini sikuiamini nilijua labda mwanhistoria huyo kachakachua kum,be ni kweli Mkwe sio kuchakachua wala nini.

Mbali na wakuchi au  "Cushites" kuwa watu Original wa Iran lakini si Iran tu  bali eneo zima la Mashariki ya kati (kama alivyoashiria mama yangu Mkwe) walikuwepo watu hawa weusi walioitwa wakushi.

Historia niliyobahatika kuisoma inasema walipatikana katika eneo kubwa la kusini mwa Egypt (Misri) karibu na eneo la mto Nile ambapo kwa sasa ni nchi inayoitwa Sudan.

Eneo hili lililokuwa na wakushi kibao si Sudan tu peke yake bali eneo hilo wasomi wanasema ni pamoja na Nubia, Wawat, Cush, Meroe na Ethiopia.

Hii inamaanisha eneo hilo lilijulikana kama eneo moja la wakushi na ardhi moja lakini kukiwa na sehemu au maeneo mbali mbali kwa maana kwamba maeneo yote hayo yalikichukuliwa kuwa eneo moja la wakushi katika kipindi kilichopita.

Kwa wamisri eneo hili walilikiita au lilikijulikana kwa jina la:"Land of the Bow".

Lakini kwa mujibu wa historia ninayoiamini ni hii inayosema kulikuwa na maeneo mawili au tuseme makabila mawili au kama sio hivyo tuseme makundi mawili kama ifuatavyo:

Katika upande wa eneo kubwa la Kaskazini (Kati ya maporomoko ya kwanza ya maji na ya nne) lilikuwa likiitwa eneo la Wawat,na katika eneo kubwa la Kaskazini(Juu ya Maporomoko ya nne ya maji) lilikijulikana kama eneo la Cush.

Wakati ule wa zama zilizojulikana kama zama za Nasaba ya 18 katika nchi ya Misri,eneo hilo lilijulikana kama eneo moja lakini lenye mikoa miwili tofauti,lakini baadae eneo hili lilichakachuliwa na hatimae kuchukua sura mpya ya mabadiliko.

Eneo la kusini baada ya mabadiliko hayo likawa ni eneo lenye nguvu zaidi,hali hii ikapelekea jina hili au neno hili Kushi kuwa neno linalopenya zaidi katika masikio ya walio wengi na likatumika zaidi na kuandikwa katika maandiko ya wamisri,na hatimae kusambaa katika eneo zima la mashariki ya kati.

Comment by Mama Malaika on January 31, 2012 at 21:12

Ha haa haa haa... huyu IL-YA nitamchapa bakora akikutupia ngumi kaka Eddie. Ha haa haaaa......... IL-YA inabidi sasa uwe unatuletea blog kama hizi na sio mambo ya siasa tunayoyasikia kila tuwashapo Aljazeera, BBC, CBS, Sky, etc. 

 

Keep it up IL-YA, each one teach one!!!!!!!!!

Comment by eddie on January 31, 2012 at 20:37

Dada Mama Malaika gazeti lako ni bora zaidi kuliko la ILYA, mtu unaona raha kusoma na unaweza kurudia hata mara elfu bila kuwa bored......ILYA samahani ni maoni yangu usitupe ngumi hahahaha!

Comment by Mama Malaika on January 31, 2012 at 20:08

Mkwe wangu IL-YA.... ujue watu wanaandika history inavyo wa-fit wao. Sie wa-Africa na weusi wengine duniani history yetu imeanza miaka maelfu na maelfu kabla ya hao wengine kuwepo (since the coming of Abraham). Hata hao Aborigines of Australia, history yao ukiifata nyuma ilikoanzia wakuta imeanzia miaka maelfu. Na kila unapotikisa mti wa history ya nchi za middle east hadi kote Asia lazima utakuta Black Civilization imeacha footprint. Na ndivyo kila ukitikisa family trees (koo) zote za Ulaya unamkuta Blackman alikuwepo na ameacha footprint yake, iwe wale mashupavu Roman Emperors or Bitish Monarchy kote kumekuwepo babu na bibi zetu weusi.

 

Original watu wa hapo Iran walikuwa ni weusi ambao ni wakushi (Black Cushites). In fact, hao wakushi walikuwepo kote middle east kabla watu weupe au wenye rangi nyeupe kuvamia Sumer (Sumeria), Susia, Elam na kwingineko ambako kote kulikuwa ni kwa hao Black Cushite Kingdoms. Civilizations zote za mwanzo (Ancient Civilizations) huko Sumer na Elam zilikuwa ni hao weusi wakushi. The ancient Elamites and Sumerians wote walikuwa ni descendants wa wakushi (Cushites). Hawa watu weupe waliovamia huko walipigana vita na hao wakushi miaka mingi, wakazaliana na hao weusi na ndio kukatokea hicho kizazi kilichokuja kujilakana kama Assyrians. Na lugha ya mwanzo iliyokuwa ikizungumzwa Iran haikuwa sio hicho ki-Farsi bali ilikuwa Cushite na Elamite. Na watu ambao hadi leo wanaongea lugha inayofanana na Elamite ni wale wa Sri-Lanka wenye ngozi nyeusi sana (twawaita Black Dravidians) wanaobaguliwa huko kwao Sri-Lanka na wa Sri-Lanka wenye ngozi ya brown kidogo ambao wanajiita wao weupe kuzidi wenzao na ndio wenye nchi.

 

Hivyo mkwe watu asilia wa Iran walikuwa ni weusi, na hao weusi hawakupelekwa utumwani na waarabu bali walikuwepo huko miaka maelfu na maelfu. Ndio maana tunaita Babylon ilikuwa mji mkuu wa the Cushite Empire of Mesopotamia. Hivi sasa duniani hii wakushi wamebakia Africa tu huko Ethiopia na sehemu ndogo ya Sudan. Na hao ndio walikuwa wayahudi wa mwanzo na sio hawa wajanja wajanja waliotoka Ulaya mashariki & US wanaojiita wayahudi. Wakushi wameandikwa kwenye vitabu vingi sana vya mwanzo iwe vya wa-Egypt, wahindi na hadi Agano la kale (Bible).

Comment by ILYA on January 31, 2012 at 19:04

Duh,Mkwe asante sana, yaani unanifanya niwe na hamu kibao bali kuongeza chachu ya kusoma hiyo Black Civilization History.

Unajua maisha ya mwanadamu bwana siku zote ni History,kama kuna mtu ni adui wa History basi huyu ajue kwamba anajiharamishia faida,maana ndugu History kusema kweli jamaa huyu kajitahidi sana kusajiri data mbali mbali na uhakika mbali mbali wa mambo ya kale yaliyopita  na hata yaliyopo, na siku zote ndugu huyu History utamkuta amekaa mkao wa kula akiwa tayari kusajiri yote yale yajayo,hakipotei kitu.

Naweza kusema asilimia 98 % ya maisha ya mwanadamu ni Historia,hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kucheki cheki History kama vile kitu:Black Civilization History,na zingine.

Comment by Mama Malaika on January 31, 2012 at 16:23

IL-YA...... Nimesoma Black Civilization History ndio nikajikuta nimeingia hadi kwenye Mesopotamia civilization na kuukuta mto Frati. Na hata huo mto Tigris nao ulikuwa muhimu sana kwa ufalme wa Assyria hapo hapo Iraq juu ya Mesopotamia. Kwenye history, nchi zote hizo jirani zilikuwa ni lands of Black Civilizations during Mesopotamia. Hao watawala wengi waliotawala Assyria & mesopotamia before Roman Empire hawakauwa Persians, Elamites, etc. na hao unaowaona leo. Baada ya Roman Empire, watawala karibu wote waliokuja kutawala hizo Kingdoms (Irag, Iran, Syria, etc.) wakawa Persians, Elamites na mchanganyiko lakini waarabu wenyewe hata siku moja hawatokubali kukwambia hivyo sababu history wameichakachua. Ukienda kwenye Museum mjini London na Berlin ndio utaona ukweli wa mambo

Comment by Mama Malaika on January 31, 2012 at 15:37

Bila ya huu mto Euphrates, Mesopotamia's civilization isingelitokea. Ni sawa na ancient Egyptian people walivyoutegemea mto Nile for their civilization. Mto huu uko hadi kwenye Old Testament (Biblia - Agano la Kale) na umesifiwa sana kwenye Biblia pamoja na mto mwingine uitwao Tigris nao uko ndani ya Iraq.

© 2019   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*