Tulonge

Huyu ndiye mgombea kiti cha Urais Jamhuri ya Czech mwenye 'tattoo' 90% ya mwili wake.

Vladimir Franz ni mmoja kati ya wagombea tisa wa kiti cha Urais Jamhuri ya Czech ambaye asilimia 90 ya mwili wake umechorwa 'tattoo'. Pamoja na hilo kura za maoni zimempa 11.4% ya kura zote ambapo amekua ni mgombea wa tatu kati ya wagombea hao 9. Franz mwenye umri wa miaka 53 ana shahada ya sheria, ni profesa wa fani ya maigizo pia ni mchoraji.

Franz alisema kuwa 'tattoo' ni jambo lake binafsi, halina uhusiano na kugombea kiti cha Urais. Pia ushindani wa kiti cha Urais siyo shindano la urembo.

Views: 1295

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on January 18, 2013 at 11:30

sema tu sio tamaduni yetu ndo maana inatutisha,nadhani nao watawashangaa wamakonde walivyojichora wakiwaona,muacheni jamaa akamue urais jamani

Comment by Dixon Kaishozi on January 17, 2013 at 16:25

kuna kamsemo kama sijachapia.. tehe.. u cant judge the book by its cover!!! Me nadhani kwanza kwa jinsi alivyo anaweza akawa bora kuliko wote kama Mama alivyosema! hizo tatoo ni mambo binafsi tu!!!

Comment by Christer on January 17, 2013 at 8:15

Mmmmh mi kwakweli kwenye picha tu ananitisha nikikutana nae live nadhani nitadondoka kwa hofu, huyo dada sijui ndo mkewe? mmmmmh, duniani kuna mambo, yaani mpaka machoni kabakiza macho ndani tu nadhani kama sehemu ya jicho isingekua delicate angepicha tatoo mpk ndani kbs ili akamilike.

Comment by Mama Malaika on January 16, 2013 at 18:43

ingawa kwa wazungu tattoo ni art na baadhi ya jamii za wazungu (vikings) ilikuwa ni tamaduni yao, huyu jamaa akiniibukia na kunishtukiza usingizini usiku wa manane sio siri kuna hatari nikapiga mayowe na kuruka dirishani kama swala, ukizingatia madirisha yetu hayana nondo. Ha haa haaaa.....

Comment by Alfan Mlali on January 16, 2013 at 17:58

hahahahahah..Duniani kuna mambo....

Comment by Tulonge on January 16, 2013 at 17:29

Asante kwa maelezo zaidi Mama

Comment by Mama Malaika on January 16, 2013 at 15:41

Muonekano wake wa nje kwa sie wengine tunaona haufai ila huko Jamhuri ya Czech inasemekana katika wagombea wote 9 yeye tu ndio msafi; yuko karibu na watu, anapendwa na vijana, anapenda democracy na ni mpigania Haki za Binadamu na amekuwa mstari wa mbele kutetea watu ambao wamekuwa wakitiwa jela kwa makosa ya uandamanaji kudai usawa, haki zao na pia kukemea rushwa na maovu ya viongozi.

Wagombea wengine wote 8 walio salia inasemekana ni mafisadi na wanatumia power kwa maslahi yao (wakiwemo mawaziri wakuu 2 wa zamani). Chakushangaza zaidi ni kwamba katika kura hizo alizozipata, wanasema hajatumia mabango au matangazo ya aina yeyote ile kwenye campaign ya uchaguzi kama wagombea wengine.

Comment by mathias mwita on January 16, 2013 at 15:07

utadhaniarnold shwaznegger kwenye picha ya predator kajipaka matope

Comment by Christer on January 16, 2013 at 12:32

Duuuuuuuuh, kwakweli hii ni ebwana ndio @ Kabegulahamza

Comment by KUNAMBI Jr on January 16, 2013 at 11:21

sasa huyu kwenye picha kubwa ya kuweka ukutani sijui ingekuaje ,maana watoto wangekua wanaogopa

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*