Tulonge

INJILI YA KALE YAPATIKANA YAFANANA NA QURAN

Nakala ya injili ya miaka 1500 iliyopita ambayo imepatikana tena ktk kanisa moja nchini uturuki  baaada ya kupotea kwa muda wa miaka mingi, ina utabiri wa kuja kwa mtume muhamad S A W baada ya masihi  issa  A S yaani yesu.

Maneno yaliyomo kwenye injili hiyo ya miaka 1500 iliyopitayanafanana sana na maneno ya Quraani tukufu na kijumla manenoyake yanakaribiana sana na mafundisho ya uislamu.

Sehemu moja ya maneno yaliomo kwenye injili hiyo yanamtaja yesu ni mwanadamu mna kumnukuu nabii huyuwa mwenyezi mungu akisema kuwa , mtume atakayekuja baada yake anaitwa MUHAMAD.Sehemu ya maneno ya injili hiyo ya miaka 1500 iliyopita yana maana isemayo,[kuhani mmoja alimuuliza masihiyesu kuhusu mtu atakayekuja kuchukua nafasiyake---Na yesu akajibu,muhamad s a w ndilo jina lake  lililobarikiwa anatoka ktk kizazi cha ismail baba yangu mwaraabu.

Waziri wa utamaduni wa uturuki pia amesema tayari Papa Benedict wa 16ametuma maombi rasmi ya kutaka wapatiwe injilihiyo iliyopatikana kwenye visiwa vya bahari ya mediterranean.

Views: 865

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Alfan Mlali on March 6, 2012 at 14:00

Ukiona hivi ujue Nabii Issa amekaribia kurudi na kuuweka ukweli hadharani..Lets keep on waiting!

Comment by Bonielly on March 4, 2012 at 17:43

bado nasikiliza nikiwa na uhakika nitakuja kuwasibitishia, kifupi  sina uhakika, nisiseme uongo mwiko,

Comment by ILYA on March 4, 2012 at 17:23

Ingawa kugundua Injili hii ya miaka 1500 iliyopita kuna athari kubwa kihistoria,lakini sinauhakika kama Uturuki imetngaza Injili hii ili ipewe  pongezi,ningelikuwa na uhakika na hilo ninge liwapongeza kwa hilo .Hivyo itabidi Uturuki tusameheane maana sitaki kutoa pongezi sehemu isiyohitajia pongezi.Kila kitu na sehemu yake.!!!

Comment by ILYA on March 4, 2012 at 0:34

Habari hii imetikisa sana huko katika safu za viongozi wa vatican,na sasa tayari wameonyesha hamu kubwa sana ya kupatiwa nakala za Injili hiyo ili wazitie macho.

Na hata viongozi  wa makanisa la Uturuki wamekubali kupatikana kwa nakala hizo bila kupinga,na sasa serikali ya Uturuki imeahidi hivi karibuni itaweka wazi nakala za Injili hiyo ya miaka 1500 zilizopita.Vyombo vya habari vya Uturuki vimedokeza kwamba Injili hii iliyopatikana imeandikwa kwa Lugha inayoeleweka na kusomeka -bila hata ya kutumia miwani-ya Kiarami.

Msomi mkubwa aliyezama zaidi na kubobea katika nyanja mbali mbali za kielimu na hasa katika Injili bwana Ihsan Uzbek, na ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa Kikristo nchini Urutuki amenukuliwa akisema kuwa: Injili hiyo iliyopatikana ni ya "zama za mtakatifu Barnaba" aliyeishi na Yesu au Nabii Issa (a.s) na ambaye alikuwa mfuasi wake bora na wa  karibu.

Injili hiyo ya kale , taarifa zinasema kwamba hivi sasa imekabidhiwa katika Jumba la Makumbusho la "Ethnografia" huko mjini Ankara ambapo itaonyeshwa rasmi hivi karibuni.

Comment by Tulonge on March 3, 2012 at 20:40

Ngoja nipite kimya kimya kwanza. Nitarudi baadae kidogo.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*