Tulonge

Jacqueline Wolper VS Amber Rose, nani zaidi kwa style hii ya nywele?

Kumekuwa na mabishano ya hapa na pale mitaani kuhusu style ya nywele za Jacqueline Wolper (Movies Super star in Tanzania) na Amber Rose (American model, artist, actress, and socialite). Ubishani huu umeanza baada ya Wolper kubadili style yake ya nywele na kufanana na zile za Amber Rose. Baadhi ya wadau wanasema Wolper amefunika (pendeza) zaidi ya Amber japokuwa yeye (Wolper) ndiye amemuiga Amber. Wengine wanadai kuwa Wolper hajamfikia hata kidogo Amber katika suala zima la kupendeza kwa style hiyo ya nywele.

WEWE UNAONA NANI ZAIDI???Views: 3569

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on March 29, 2012 at 12:56

Manka na Boni mmenifurahisha sana ingawa mi kwa leo napita ntarudi kutoa yangu ya moyoni.

Comment by manka on March 28, 2012 at 18:10

@ Ilya habari zote huwa mimi nazisoma na ukianaglia kwenye coment utaona nimecoment, ki ufupi wenzake ambao wanamsema vibaya ni wivu tuu, japo hakuna bninadamu mkamilifu.

Comment by ILYA on March 27, 2012 at 18:09

Manka@lakini mara nyingine unajua mtu ukionyesha juhudi fulani kuliko wenzako wenzako wanaweza kukuponda kwa kuwa umewazidi sifa na kiwango.

Wolper naamini anaweza kuwa anapondwa na wasanii wenzake wa kike wanaomuita Malkia wa uongo kwa kuwa Wolper anatoa michango mbalimbali ya wasanii wenzake na anasaidia zaidi kuliko wananii wengine katika matukio yanayohitaji michango ya wanajamii kama vile kuchangia waathirika wa mabomu yaliyotokea Gongo la Mboto.Mwenye anathibitisha hilo kw akusema anaonewa tu na wasanii wenzake wa kike.Binafsi siko mbali kukubaliana na madai yake.

Tazama picha kisha link ifuatayo:

http://www.globalpublishers.info/profiles/blog/show?id=5398006%3ABl...;xg_source=activity

Comment by ILYA on March 27, 2012 at 17:58

Manka@ ni kweli hujaona,na ni vigumu wote kuona uongo wa mtu,ila wale walio karibu ya mtu wanaweza kuuona haraka,miongoni mwa watu wanaoweza kuthibitisha uongo wake ni mwanadada LULU,ambaye ni msanii maarufu kwa bongo,na ni msani ambaye anafanya kazi kisanii na wolper katika picha za kibongo.

Lulu huyo ndiye anasema Wolper ni malkini wa uongo,hilo jina limesikika kwa wengi lakini lulu amethibitisha kuwa anayekusudiwa kw ajina hilo ni wolper.Na waasanii wengine tofauti na Lulu wanathibitisha kuwa hilo ni sahihi hiyo ni sifa ya Wolper.Tazama picha ifuatayo kisha tembea usome zaidi kuhusu hilo kwenye link hii: http://www.globalpublishers.info/main/search/search?q=malkia+wa+uongo:

Kuhusu yeye na Diamond, unaweza kutambaa na link hii baada ya kutizama picha hii:

http://www.globalpublishers.info/profiles/blog/show?id=5398006%3ABl...

Kuna wakati alidai kuwa anatumia laki tatu kwa siku,siku moja alidakwa akila ugali kwa kulumangia na kachumbari;hii inamaanisha siku hiyo laki tatu hazikufika.!!!!

Tazama picha hii:

Alihongwa gari siku za nyuma,lakini akadai kuwa hilo gari kapewa na mjomba wake,baadae akaja kukiri kuwa ni la kuhongwa na sasa kasha yaona madhara yake na kwamba hatarudia tena kuchukua chukua magari ya kuhongwa na kwamba sasa anapambana kuhakikisha anajimilikisha vya kwake

Tazama picha na link :http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/wolper-sitakubali-t...

Ingawa hilo la uongo si sehemu ya maudhui kwa hapa,ila habari ndio hiyo kama hiyo tabia ni yake inafa ajirekebishe maana itaharibu kabisa umaarufu wake unaweza kuishia katikati.Maana haingii akili wakuite Malkia wa uongo hivi hivi tu.!!

Comment by manka on March 27, 2012 at 13:32

Ilya sijaona uongo wa WOLPER sasa kama alikuwa hatoki na Diamond aseme anatoka naye kwa sababu magazeti ya udaku yameandika? pili umaarufu wao hauwezi kulingana kutokana na utofauti pia wa nchi wanazotoka wolper ni wa hapa hapa mavumbini na  Amba ni wa huko magorofani, lakini kibongo bongo Wolper kati ya wasanii wa bongo yupo juu, kwani tayari mjengo wake upo kwenye finishing anakokota mkoko wa 25 million tofauti na ule wa 8 milliion aliokiri kuhongwa, anabiashara zake ambazo zinafanya vizuri tu. kwa ufupi kibongo  yupo juu kuliko hata hao wanaojiita wa mjini skendo zao kubwa za mabwana.

Comment by Bonielly on March 27, 2012 at 11:34

hapa imeelezea style ya nywele tu, tuacheni sifa zake nyingine, kama angeelezea kwamba wanashindana kwa sifa gani, kwanza tungechunguza sifa za hawa wote, halafu ndio tuanze kutoa makosa, mimi naona wote 50% kwa 50%

Comment by ILYA on March 26, 2012 at 20:45

Ee bwana kaka Tulonge@,hapa lazima mtu uwe muwazi,Wolper kafunika ingawa amber anamzidi umaarufu,lakini na yeye kamzidi kwa kujilemba na usmart uliochanganyika na ucute.

Comment by Tulonge on March 26, 2012 at 20:04

Duh! ili kiukweli Wolper amefunika. Amependeza sana, nimeamua niwe muwazi.

Comment by Alfan Mlali on March 26, 2012 at 17:32

Duh..Huyu Jack kumbe ndio mzuri hivi...mi huwa nasikia tu stori zake ila sikuwahi kumuona.. Yuko juu and sexy.

Comment by Tulonge on March 26, 2012 at 14:31

Hhahahahahaaa "Malkia wa uongo". Chalii umenifurahisha sana. Naona mnamfagilia mbongo mwenzenu

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*