Tulonge

Jamaa wakiiba mafuta toka kwenye tanki la lori mchana kweupee eneo la Tazara DSM

Bila wao kutambua, Kamera ya Tulonge iliwanasa vijana hawa watatu wakiiba mafuta toka kwenye lori la mafuta lenye namba T873 BHE eneo la Tazara barabara ya Nyerere DSM leo. Vijana hao walipata fursa hiyo baada ya lori hilo kusimama likisubiri taa za kuruhusu kuondoka. Kwa muda wa dakika chache, vijana hao walifika kwenye lori hilo na kufungua midomo ya tanki na kuanza kukinga mafuta kwa kutumia mifuko ya nailoni. Haikufahamika kirahisi walitumia nini kufungua midomo ya tanki hilo.

Vijana wakiendelea na wizi huo bila wasiwasi

Baada ya lori kuanza safari na wao walisitisha zoezi na kuanza kuondoka

Views: 1080

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by CHA the Optimist on January 27, 2014 at 19:24

Ha ha ha! Dismas, I will press charges against you---kwa maana umenisingizia.

Comment by Tulonge on January 27, 2014 at 18:44

Halafu huyo mwenye kofia siyo Cha jamani? au macho yangu

Comment by CHA the Optimist on January 27, 2014 at 17:28

Asante Dixon, asante Zainabu, na asante Omary!

Wajua tunaoneana aibu sana ambazo kiukweli hazina manufaa!

Tuna unafiki ndani yetu ndio maana tunasita hata kuwaambia ukweli wa mambo watu kama hawa-- kuwa wanachofanya si sahihi, na wala hakitawasaidia kwa maisha yao yote zaidi ya kuwa "figure of fun".

We need to change our society.

Comment by Dixon Kaishozi on January 27, 2014 at 9:08

Kaka CHA the Omniscient... hehehehee.. na mimi nimeliweza hilo jina kama kaka Omary... 

Naunga mkono wazolako kwa 50%.. Kwani hao vijana kiujumla ni wavivu tu wa kujituma na ufinyu wa kufikiria. Nadhani suluhisho ulilotoa la kuwaweka jail ni bora kuliko kwenda kupoteza zana za kilimo kwa watu wenye akili kama yao!! Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo.. 1. hao hawajapenda kujishughulisha ndiyo maana wanafanya hivyo ili SIKU IPITE na si kwa malengo ya mbeleni. 2 - Si wote ambao utawasaidia njia hiyo wakapenda kwenda kuweka kambi porini kwa miaka mitatu.. washazoea kula bata mjini..

Mwisho kuna kijana alikua wa mtaani hapa arusha, akapata ufadhili wa kupelekwa shule, mahala pa kulala, chakula na zana za mafunzo!! Mwisho wa siku alitoroka na kurudi mtaani kwa madai maisha aliyopewa hayawezi na kawamisi masela wake kwani walipigwa stop kumtembelea na yeye kuwa nao!!!


Sasa kijana kama huyu hata ufanyaje... na suluhisho ni kumuweka magereza tu akajifunze ujasiliamali huko kuliko kumuacha mtaani kama kibaka!!

Comment by Omary on January 26, 2014 at 10:18
CHA the Omniscient hahaha leo nimeliwezea jina lako, mie nimependa mtazamo wako unaleta maendeleo hata kama ni mimi ndio unipe hizo nyenzo ningekybali kujifungia shamba najuwa ndani ya huo muda uliopanga nami maisha yangu yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana, je lawama litupwe wapi? kiukweli tatizo la ajila ni sugu Africa naviongozi hawajali wabatowa agadi wasizoziweza wa kutimiza sasa angalia nguvu kazi inavyopotea bure ksma hao wanatumia nguvu nyingi wanapa mafuta kidogo huo muda wangeutumia shamba wangebadilisha maisha yao.
Comment by Zainabu Hamis on January 25, 2014 at 18:31

CHA The Omniscient, sasa tutakuita dictator. Natania kaka yangu, usije nianzishia mashambulizi mie!

Good Idea, japo kwa wengine litaleta hisia mbaya.

Comment by CHA the Optimist on January 25, 2014 at 18:11

Huwa nawaona mara nyingi sana hawa jamaa hasa pale Tazara na maeneo fulani ya Buguruni. Hawa ukiwauliza kwa nini wanafanya hivi.....nafikiri watakujibu "kazi hakuna". Lakini kiukweli, kazi kweli ni tatizo, si tu katika Tanzania yetu ya Nyerere, bali ni kutoka Angola hadi Zimbabwe ya Mugabe, Robert kazi ni tatizo. Mimi kwa maoni yangu watu kama hawa ni wavivu wa kufikiri, hapa swali la kujiuliza ni Je, kazi hii wataifanya mpaka lini? Je, kazi hii itawafaidia nini maishani---na hii sio kazi wadau, samahani.

Ningekuwa na uwezo hawa jamaa, ningewakamata na kuwapeleka huko interior, na kuwagawia eneo la hekari zisizopungua mia moja, ningewapa chakula cha kula kwa miezi sita, na mahitaji yote muhimu ya binadamu, ningewakabidhi trekta ama zana za kilimo, ningewajengea nyumba ndogo ya kuwatosha kuitumia kwa shughuli zao za kilimo. Na mwishowake ningewaambia tu kuwa sitaki kuwaona nje ya kambi hiyo, kwa kila wakati itakapofanyika patrol. Na ningewaambia vilevile kuwa zana za kilimo inatakiwa wazilipe ili zije kutumika na wengine kama wao, ningewaambia vilevile kuwa--ili warudi mjini--basi ni lazima ipite miaka isiyopungua mitatu. Na iwapo itatokea wakakiuka agizo hilo, basi ni Jail kwa miaka isiyopungua mitano na kazi ngumu zaidi ya hiyo kambini.

Haya ni mawazo tu wadau, sio sheria!

Comment by KUNAMBI Jr on January 23, 2014 at 9:46

haha haha masela wenzako wako dis bangi mbaya jaman mweee

Comment by Mntambo Mburi on January 21, 2014 at 16:51

Wakati mwingi magari haya huwa yameshashusha mzigo (discharging) hivyo vijana hawa huambulia mafuta machache yaliyobaki kwenye matanki. Shughuli hii huifanya huku madreva na utingo wa magari hayo wakifahamu kabisa, na pengine ni kwa ruhusa yao hufanya kazi hii.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*