Actress and former miss Tanzania Wema Sepetu kama kawa ameshuka na mpya ya kumpulizia mbwa wake aitwaye Fiona pafyumu yenye thamani ya dola 120 (zaidi ya shilingi 180,000).Mkali huyo asiyekaukiwa na matukio Bongo amefunguka kuwa analazimika kumgharamia mbwa huyo pafyumu hiyo kwani ni moja kati ya viumbe ambavyo anavihusudu kupita maelezo.“Lazima anukie kama mimi ninavyonukia, pafyumu humfanya anukie vizuri hata ninapokuwa nimetoka naye mitaani naye anaonekana kweli ni mbwa wa staa,” alisema Wema. Kuhusu manunuzi, mkali huyo anayekimbiza kwenye soko la filamu Bongo alisema mara nyingi pafyumu hizo huwa anaagiza kutoka nje au kwa watu wake maalum hapa Bongo ili kuwa na utofauti wa ubora na hadhi yake ya kistaa.
Chanzo: Audifacejackson Blog
Add a Comment
Halafu watu wa tabia hii ukute nduguze wa karibu hasa mabinamu zake wanasota kununulia watoto daftari za shule au viatu wakati yeye atumia 180,000 ajili ya perfume kupulizia mbwa, na hapo bado chakula cha huyo mbwa na kurambishwa ice-cream za bei mbaya kama wafanyavyo celebrities wenzie wa ulaya aliowaiga
kawaida ya wabofongo,wakati watoto wa watanzania wanakufa njaaa,hawana elimu wala matibabu bora eye anatenda matendo kama hayo,Eee Mungu tusaidie watanzania tubadilike
Inaelekea hako KADOGI KANAMDUUU!!!!!!
kweli mwenda hiyo cop and paste
wame copy na ku paste
Usista duu mwingine hauma maana
Halafu hiyo kuwa na hicho kijibwa ndio wanawaiga kina Paris Hilton nini? Nimeshangaa last time nilipokuja Tanzania niliona wadada pale Mikocheni shopping centres wamebeba vijibwa vidogo vidogo nikajiuliza kulikoni? Haikuwepo hiyo Tanzania miaka ya nyuma.
Ulimbukeni ni kitu kibaya sana duniani.
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge