Tulonge

Kenya:Mwanafunzi wa miaka 90 aendelea na masomo yake vizuri.Sasa yupo darasa la 3.

-Ameahidi kuendelea na masomo endapo Mungu atamuwezesha kuendelea kuona.
-Anapendwa sana na wanafunzi wenzake darasani,ambao ni kama vitukuu kwake.
-Huwaongoza wanafunzi wenzake kusoma wawapo darasani.

This is the story of a 90-year-old grandmother who is just in standard three. Priscillah Sitienei or 'gogo' as her she is popularly known, can now read and write. And she has even picked up a few popular English phrases. NTV's Rita Tinina who had visited her early last year, went back to see how she is doing

Views: 351

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on March 1, 2012 at 16:54

Watu tumezaliwa kukulia mazingira na nyakati (era) tofauti hivyo hatujui sababu gani ilichomfanya bibi asipelekwe shule alipokuwa mdogo miaka hiyo ya ukoloni ya 1920s to 1930s kabla hajaolewa.

Wameshakuwepo wengine wenye umri wa miaka 80 hadi 100 kuhudhuria masomo duniani ingawaje wengi ni wanafunzi wa Secondary Schools na vyuoni na sio Primary Schools. 

Wataalamu wanasema kuwa kuna faida kubwa kwa wazee kujihusisha na masomo/kusoma kwani kuna slow down progress ya ugonjwa wa Dementia (matatizo ya akili yanayotupata uzeeni). Bibi huko darasani akiwa na hao watoto wadogo anaendeleza communication and reasoning skills kitu ambacho ni kizuri kwa afya ya ubongo wake na akikaa nyumbani hatopata mtu atayekaa naye muda wote.

 

BONIELLY.... mtu asikudanganye na wala usikate tamaa, ukipata muda wewe soma hata kama ni kitu tofauti na kazi unayofanya (hata iwe masomo ya jioni) kwani unakuwa multi skills.

Comment by ILYA on March 1, 2012 at 16:03

Hii ishu ya Bibi naweza kuipatia anuani hii:

"Ujinga ni adui wa mwanadamu na Elimu na maarifa ni rafiki wa kweli wa mwanadamu":

Kwa maana kwamba:

Elimu ya mama huyu katika uzee wake ,ikiwa atabahatika kujua kusoma na kuandika, basi inaweza kumasaidia bado na  hajachelewa.Mfano:

Ataweza kusoma vitabu mbali mbali na hasa vile vitabu vya dini kama Bibilia na Qur'an.Ataweza kuelewa katika sentensi hi Mwenyeezi Mungu alikusudia kutufikishia wanadamu ujumbe upi au funzo lipi au maelekezo yepi,kisha kutafakari na kufanyia kazi kama inahitajika kulifanyia kazi.

Bado hiyo nayo ni faida moja wapo unayoweza kuipata kupitia kujisomea mwenyewe bila kusomewa na mtu,maana vitabu hivi vya Mungu vimejaa sana hekima na mwongozo na ushauri mbali mbali kwa mwanadamu ,na hekima hiyo kutoka vitabu hivyo mtu anaihitajia wakati wote hata ule wakati wa uzeeni.

Hivyo kwa asiyekuwa kuwa na elimu ya kujua kusoma kilichoandikwa hataweza kujichukulia hekima na mwongozo yakiwemo mafunzo yaliyomo ndani ya vitabu vya Mungu Muumba.Na kujisomea mwenye ni tofauti sana na kusomewa na mtu,anaesomewa na anaejisomea,wawili hawa hawalingani ubora na hata kw aupande wa upataji wa faida watatofautiana sana.

Hivyo Bibi huyu anamaanisha anachokimaanisha katika kusoma kwake!.Hilo mosi:

Pili, kusoma bado ni "sehemu ya maisha",na mwisho wa maisha ni pale unapotengana na dunia.

Hivyo kwa mtu ambae bado ana roho na aendelea kuishi bado,si mbaya akiishi hata sehemu hii ya maisha iliyobora,nayo ni kusoma.

Na hapo usisahau kuwa  ujinga siku zote ni adui wa mwanadamu!,hivyo mwanadamu utamuona siku zote akimchukia adui yake na kujaribu kujitenga nae,na chuki hii dhidi ya adui yako inaendelea hadi uzeeni,yaani si kwamba ukizeeka unakuwa na mapenzi na adui yako,hapa bali utazidi kumchukia tu,hayo ni mambo ya kinature.

Hivyo ujinga  ni miongoni mwa adui wa mwanadamu,na mwanadamu atazidi kumchukia adui huyu tu hata akiwa na miaka dahri!!.

Na ndio maana utaona mtu afanya awezalo kujiepusha na adui yake kwa kuwa hana alitegemealo lolote la faida kutoka kwa adui huyo,maana adui yako siku zote yuko "against wewe",na kinyume chake huyo hataitwa adui.

Hivyo mwanadamu atafanya awezalo kumtafuta rafiki wa kweli,nae ni Elimu,na Maarifa.

Tuko pamoja!.

Comment by Bonielly on March 1, 2012 at 10:59

lkn anatukumbusha tusikate tamaa kielimu kwani elimu haina mwisho, niliwahi kusikia hilo neno lkn sasa ndio naamini,

Comment by manka on March 1, 2012 at 9:30

HII INA MWEZESHA YEYE KUWA NA KITU CHA KUJISHUGHULISHA, NA HIVYO KUONDOA USUMBUFU KWA WANAO MTUNZA.

Comment by manka on March 1, 2012 at 9:28

saafi sana bibi, endelea hivyo hivyo, ELIMU HAINA MWISHO.

Comment by Dixon Kaishozi on March 1, 2012 at 8:56

Nisimkatishe tamaa ila kwa upande mmoja au mwingine.. hicho ndicho anachoweza kufanya kwa sasa.. kwanza kupata "attention na support " kutoka sehemu mbali mbali ali aweze kujikimu kimaisha.. hakuna lolote hapo na shule!! alikuwa wapi kipindi kile ? angekuwa na umri huo anatafuta P.h.d , digrii ya 15 hapo ningekubali kwamba bibi huyu anauchungu na shule kweli kweli ila siyo a, e, i, o u !!

Comment by ILYA on March 1, 2012 at 0:43

Soma hata kama una miaka 100 !!

Kusoma kuna faida kubwa sana,iwe umri wa ujana au uzee.Kwa ufupi unapokuwa na umri mkubwa (uzee) kitu ambacho unaweza kukifanya ili uendelee kujiseti fiti kiafya na kuupa mwili nguvu ya kuwork ni kusoma namna hii.

Hivyo usomaji wa uzeeni lazima uzingatiwe na uzee usifanywe kuwa mwisho wa kuhitajia elimu bali umuhimu wake (Elimu)ubakie pale pale kwa kuzijumuisha nyakati zote za ujana na zile za uzee.Na hakutakiwi kuwepo na aibu katika hili.

Mwanadamu ni mnyama wa jamii na hatakiwi kujifunga kwa kujiwekea mipaka.

Na Kitu "umri" hakina uhusiano wowote na lile jambo ambalo Mwanadamu anahitaji  kulifikia.
Hivyo basi,kwa mtazamo wangu:Elimu katika umri wa uzee ni moja ya njia za kuhakikisha kwamba:

"Mtu anaweza kufikia (au kufanya lile) jambo ambalo siku zote alitaka na kutamani kulifikia/kulifanya,na elimu hiyo itamfanya mtu binafsi kujiamini kuwa hakika yeye si mbaya na si mjinga kama alivyokuwa akijidhania hapo kabla.

Mwenye hekima mmoja (na bila shaka Mtanzania huyo) alisema:

"Elimu ni akiba iliyo bora zaidi kwa ajili ya umri wa uzee".

Hivyo hata mtu akitaka kusoma akiwa na umri wa miaka 50 au 60 au 90 au 100,itakuwa ni vizuri sana na hajafanya kitu hatari wala chenye madhara.Maana elimu kwa kiasi kikubwa inachangia bali ni faida kubwa kwa upande wa afya yake.

Hivyo hiyo nayo ni faida moja wapo ya elimu,"kwa mana kukomaza afya ya mtu", ukiachilia mbali faida zake zingine.

Note:"Old age education can also be a way of living".

------------------------------------------

Tuko Pamoja!

Comment by Tulonge on February 29, 2012 at 23:00

Kweli elimu haina mwisho. Ana moyo sana bibi huyu,sitaki kuandika maneno ya kumkatisha tamaa teh teh teh!

Comment by BARAKA FRANCO CHIBIRITI on February 29, 2012 at 22:54

Ili iweje? Akifika kwa Mwenyezi Mungu awe msomi au?

Comment by Mama Malaika on February 29, 2012 at 21:46

This is awesome! Gogo anipa matumaini niendelea kusoma

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*