Tulonge

Kijana ajiua kwa kuchoshwa na matezo ya Ukimwi

Kijana mdogo wa miaka 18, mkazi Dar es Salaam, Abdallah Salum, amekutwa amejinyonga chumbani kwake akidai amechoshwa kusumbuliwa na ugonjwa wa Ukimwi.


Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema jana kuwa Salum, mkazi wa Charambe wilaya ya Temeke alikutwa amejinyonga juzi kwa kutumia kamba ya katani aliyoitundika kwenye kenchi.
Alisema kijana huyo aliacha ujumbe uliosema; “ugonjwa huu wa Ukimwi umenisumbua sana.”


Kamanda huyo alisema mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Temeke na sasa unafanyiwa taratibu za mazishi.


Habari za kijana huyo kuchukua uamuzi huo zimewashangaza wengi wakihisi Salum alikuwa hafuati masharti wala kutumia dawa za kurefusha maisha kwani wanaofanya hivyo siku hizi ‘hawateswi’ na magonjwa yanayosababishwa na mtu kuishi na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi (VVU).


Wakati huo huo, mkazi mwingine wa Boko wilaya ya Kinondoni, Humphrey Stanley (35) alikutwa amekufa chumbani kwake baada ya kujinyonga kwa kutumia mkanda wa begi alioufunga kwenye kenchi.


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema chanzo cha mtu huyo kuamua kujinyonga hakijafahamika kwani hakuacha ujumbe na polisi wanaendelea na uchunguzi. Mwili wa Humphrey umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.


Katika tukio jingine, mtu aliyetambuliwa kwa jina la Andrew Charles mwenye umri kati ya miaka 25 na 30 amekutwa amekufa ndani ya gari Magomeni Makuti jijini.


Kamanda Kenyela alisema mtu huyo amekutwa amekufa ndani ya gari aina ya BMW lenye namba za usajili T 585 AFN, chanzo cha kifo chake hakijafahamika na mwili umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Chanzo: ziro999.blogspot.com

Views: 576

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on January 3, 2013 at 11:22

WALIOJINYONGA WAMEAMUA KUJIWAHIA NAFASI

Comment by nestory solile on December 29, 2012 at 18:44

its balance of nature brother.kila mtu kapangiwa kapigo kake, but im sorry kwa members kama kuna mtu kati yetu anao then asisite kunitaarifu ili nimpe mbinu mbadala ya kufa na siyo kamba.mungu ampumzishe kwa aman amain.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*