Tazama kina dada walivyo na roho ngumu hawa. Hawana hata uoga, wamemchanganya muuzaji hadi kaingia kingi.
Add a Comment
@ mama Malaika mimi huku hoi ha ha ha @ mlimani city kuna wezi sana kina dada pia nataka kukwambia kuna wakina dada pale kazi yao kubwa ni kujiuza pia ukimwona anafanya window shopping akimwona mwanaume anamkonyeza sasa ukiwa bwege unakubali kutoka naye lol panatisha pale. mimi nikienda pale nafanya kilichonipeleka haraka natoka kuendelea na kazi zangu wapo watu wengi sana idle maeneo yale ya mlimani city.
Hapa kunakuwa na watu kwenye kijichumba kazi zao ni kuangalia hizo CCTV hivyo mtu akiiba wanakuwa wanamuona.
Hawa wadada ni wezi kweli halafu huwezi wazania, nasikia Mlimani City kuna wezi sana kina dada.
Mmmm..inavyoonekana kama hawakukamatwa hawa na hii video imetafutwa baada ya yule dada kwendas kureport kuwa kaibiwa..Huku bongo watu wanaweka CCTV camera lkn hakuna mtu anayekaa kuziangalia mpaka litokee tatizo ndio tuka-play back. Hata Hapa ofisini kwetu tumeshalizwa simu mara mbili moja receiption na zingine kwa branch manager..Baadaye tukichek kwenye camera ndio tunawaona wezi lkn haisaidii maa wanakuwa wameshasepa kitambo sana..
yani mpaka mwili wangu umesisimka, duu, hawa mademu makauzu kuliko daaga,
Duh! kaka Eddie ndio maana waingereza wanawachukia sana Romanians & Bulgarians.
Dada kweli wengi wanatoka Eastern Europe, hao waliojikata vidole wanatoka Romania.
Ndiyo maana Romania na Bulgaria wanasita kuzikaribisha wawe full time members wa EU.
Sasa hivi Holland na Finland zimeweka veto kutokukubali wawe wanachama kamili!
Kuna hata wizi wa kuiba pesa za watu kwenye ATM. Inawekwa camera kwenye hizo machine na wanaiba codes na kila kitu! Baadaye inatengenezwa bandia!
Njoo London, nenda New York hadi Tokyo Japan watu kama hawa utawakuta. UK hivi sasa inatwa the Capital of Shoplifters in Europe sababu kuna wageni wengi mno na shoplifters wengi ni wageni toka nchi za Ulaya mashariki, Russia na kutoka Asia hasa nchi ya uchina.
Kwa kawaida wizi wa aina huu upo sana Europe. Kuanzia shop lifters hadi pick pocketers...hadi robbers!
Na siku hizi wako wale wanaitwa professionals!
Yaani kazi zao ni wizi wa kiaina....wengi wao ni wale wabugia unga (drugs) ili wapate pesa za kununua dose!
Niliona kwenye tv reportage moja jinsi walivyo creative katika wizi.
Kuna jamaa alishikwa kwa camera....alichukua box kubwa la kama kilo 20 za sabuni ya unga( washing powder) alichana hilo box kwa chini baadae akachukua laptop akaiweka humo kwenye box. Akaifunga vizuri na kwenda counter kulipa hiyo washing powder.
Jamaa wa security wakamshika baada ya kulipa.
Vile vile walionyesha kundi la pick pocketers...yaani jamani nilishikwa na bumbuazi jinsi walivyokuwa organized...unakuta hata mtu anakata vidole ili mkono uingie vizuri mifukoni du!!!
Na huwezi kuamini kwamba wanavaa vizuri na kujipodoa na wengi ni wanawake...kwa sababu ni vigumu sana kuamini kwamba mwanamke anaweza kuiba hasa ukiona amejipodoa.
Kuna ingine kali zaidi jamaa aliiba gari show room.....alikuja kukamatwa mpakani na hilo gari..
Unakuta mtu ameweka D&G sasa wewe umevaa Kaunda suti yako, mwite huyo mwizi badala yake watakushika wewe kuwa ni mwizi!
Dadangu olivia tatizo hapa si kuwa tajiri ama kuwa na uwezo wa kuyapata mahitaji fulani,issue hapa ni tabia ya mtu binafsi na si umaskini wake ama utajiri aliona.ni kwelikbs kina dada mmekuwawadokozi sana wa vitu vidogovidogo ambavyo havina mantiki yoyote kwao na familia yake
Duh.dada Olivia hiyo kali kuliko hii kwenye kideo.!!Mtu tajiri kisha anakubwa.Sasa si kapata hasara hizo cheni zake zimeondaka kirahisi jamani!,au nazo alikwiba si za kununua!!!.
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge