Tulonge

Liberatus Barlow: Mwili waagwa Mwanza; Salam za rambirambi za Rais Kikwete


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa mno na mauaji ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Barlow yaliyotokea usiku wa kuamkia juzi mjini Mwanza.

Katika salamu za rambirambi alizompelekea Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspeka Jenerali Saidi Mwema, asubuhi ya leo, Jumapili, Oktoba 14, 2012, Rais Kikwete ameagiza jeshi hilo kuhakikisha linachukua hatua za lazima kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria watu wote wanaotuhumiwa kupanga na kutekeleza mauaji hayo.

“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ACP Liberatus Barlow kilichotokea usiku wa Ijumaa katika jiji la Mwanza ambako watu wasiojulikana walimpiga risasi na kumwua ofisa huyo mwandamizi wa Jeshi letu la Polisi.”

“Historia ya ACP Barlow ni historia ya mfano katika utumishi wa umma na hususan katika Jeshi la Polisi. Kwa hakika, Jeshi la Polisi limempoteza kamanda hodari na wananchi waTanzania, hususani wale wa Mkoa wa Mwanza, wamempoteza mlinzi shupavu wa usalama wao na mali zao,” amesema Rais Kikwete katika salamu zake na kuongeza:

“Nakutumia wewe IGP salamu zangu za rambirambi kufuatia mauaji hayo. Kupitia kwako nalitumia Jeshi zima la Polisi pole zangu kwa kuondokewa na mwenzao na katika mazingira yenye kutia uchungu sana. Aidha, kupitia kwako, naomba uniwasilishie salamu zangu za dhati kwa familia ya ACP Barlow ukiwajulisha kuwa niko nao katika wakati huu mgumu sana. Naungana nao katika kuomboleza kifo cha baba yako na mhimili wa familia yao na katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amen.”

Rais Kikwete pia ametumia nafasi hiyo kulitia moyo Jeshi la Polisi. “Kitendo hiki ni kazi ya watu waoga lakini nawasihi kitendo hicho kisiwakatishe tamaa katika kutekeleza wajibu wenu na kufanya kazi nzuri ambayo mnaendelea kuifanya katika nchi yetu ya kulinda usalama wetu na mali zetu,”

Ameongeza: “Badala yake kitendo hiki cha woga kiwahamasishe kuongeza kasi ya kudumisha usalama wa nchi yetu. Na kwa kuanzia, tuhakikishe kuwa wote walioshiriki katika kupanga na kutekeleza mauaji hayo wanakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.”

Chanzo: GSsengo blog

Views: 1199

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on October 18, 2012 at 10:10

Napenda sana kuchezea haya madude "Guns".. tehehehee.. Maana tunakoelekea karibu kitanuka!!! @ Mama M. Hapa arusha kuna kambi moja ya jeshi ya monduli, wana uwanja mzuri sana wa kufanya shooting.. mkitia timu tu mi nawapeleka huko!!

Comment by Mama Malaika on October 17, 2012 at 18:38

Dixon kumbe huwa waenda lenga shabaha.. baba Malaika ndio zake hizo hadi Sniper Rifle and Minigun. Tukija bongo akikutana na wewe naona mtaelewana sana sana maana shooting ndio hobby yake. LOL..... Mie nataka ajili ya ulinzi maana hali si nzuri maeneo yetu tuishio Dar, majambazi vijana wenye mapanga wamekuwa wakiingilia wakazi na kusafisha nyumba nzima, nasikia imekuwa kama mchezo siku hizi. Majambazi wengi wajanja wanajua bunduki kwa ku-isikilizia milio inapofyatuliwa, iwapo jirani akifyatua machine kali wanakimbia

Comment by Samwel Mnubi Masatu on October 16, 2012 at 23:51
kama dda alyekuwa na huyu kamanda hafahamiki kuwa alikuwa ndugu yake bas kumbe alkuwa dem wake na jamaa alikuwa anatoka kupalilia bustan ya eden!
Comment by Samwel Mnubi Masatu on October 16, 2012 at 23:51
kama dda alyekuwa na huyu kamanda hafahamiki kuwa alikuwa ndugu yake bas kumbe alkuwa dem wake na jamaa alikuwa anatoka kupalilia bustan ya eden!
Comment by Dixon Kaishozi on October 16, 2012 at 16:25

Lakini unampango wa kwenda Afghanistan ? @ Mama M

Comment by Dixon Kaishozi on October 16, 2012 at 16:23

Jumapili ijayo tunaenda kwenye kulenga shabaha, huko tunakuta watu wengi wenye "connection" mbalimbali hivyo nitakuulizia alafu nitakupa jibu!! @ Mama M!

Comment by Mama Malaika on October 16, 2012 at 16:18

Dixon... vipi naweza kupata Minigun (M134)?

Comment by Dixon Kaishozi on October 16, 2012 at 15:54

Usipochukua hatua mapema utajuta!! hahahaa.. Nitafute kwa wakati wako nitakupa mchongo umiliki moja!! @ Dismas

Comment by Tulonge on October 16, 2012 at 14:49

Dixon kama zinapatikana kirahisi pande hizo inabidi nije nichukue moja.Kuna vijamaa vimeanza kuzunguka zunguka mitaa ya home, nadhani vinamdundia Doreen wangu. Walahi nikiipata hiyo nawatandika ya kichwa.

Comment by Mama Malaika on October 16, 2012 at 14:42

Hata mie nashindwa kuelewa, mara ya kwanza walisema alikuwa katoka kumpeleka dada yake, mara sio dada yake.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*