"Deffy na Sarinya alikuwa pamoja kwa miaka 10, na hatimaye waliamua kukaa chini. Walikuwa wameahirisha harusi mara kadhaa, kutokana na kutokupata muda muafaka na ukweli kwamba Deffy alitaka kumaliza elimu yake kabla ya kufunga ndoa. Hata hivyo, baada ya kifo cha mpenzi wake Sarinya Deffy aliona hakuna kizuizi cha yeye kutimiza shauku yake ya kufunga harusi na mchumba wake huyo, hivyo aliamua kufunya harusi kabla ya kumzika. Sherehe hiyo ya Kibuddhist ilifanyiaka katika mji wa Surin kaskazini mwa Thailand.
Deffy alisema mbele ya jamaa na marafiki waliokuwepo katika sherehe kuwa ibada hiyo amefanya ili kuonyesha upendo wake mkubwa kwa Sarinya. Marafiki na jamaa kadhaa walihudhuria harusi hiyo, na tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi nchini humo na kufanya TV ya taifa ya nchi hiyo kurusha tukio hilo live. Hadithi, pamoja na picha kutoka kwenye harusi hiyo sasa vimevuta hisia za watu wengi katika internet, hivyo kuzua mijadala kadhaa. "
Kwa hisani ya "Mtandao"
Add a Comment
mapenzi bwana kila mmoja anapenda anavyohisi,
RIP Sarinya. Hapa siwezi sema mengi maana hayajanifika. Mungu ni mwema atamsaidia na kumpa nguvu huyu kijana kuendelea na maisha yake
Ni mapenzi yalopitiliza, ila wanadamu tumeumbwa kusahau, atasahau atapata mpenzi mwingine na ataoa
Huu upendo ulipitiliza na kuwa uchizi sasa
Mijimambo ya kimaajabu kama hii mara nyingi hutokea kwenye vijinchi vya huko Ng'ambo.Lakini enewei inaonekana huyu kijana alikuwa ana mapenzi ya kweli kabisa kwa mupenzi wake.Mungu amhifadhi ndugu marehemu,na ampatie kijana huyu moyo wa subira,asije kwenda kumfukua kaburini.!!
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge