Tulonge

Madaktari 72 Watimuliwa Kazi -MBEYA

Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara Aikzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi kwa madaktari hao.

BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.

Imeelezwa kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya.Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo
la 2009 kifungu namba F.16-F17 na F. 27.

"Hivyo kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu,"alisema Sigara.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi
19(Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.

Alisema, kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns
doctor 54 na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012
ambapo tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura
kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa
uamuzi.
Sigara, aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.
Alisema, baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi

"Iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,"alisema.

Aidha, alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.


Chanzo: http://mbeyayetu.blogspot.com

Views: 259

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on June 30, 2012 at 21:18

TZ imekula hasara hasa ukizingatia nchi baadhi za west (UK, Canada & Australia) zina upungufu wa medical professionals (doctors & nurses). UK government imeanza mchakato wa point system kupata doctors toka nchi Jumuiya ya Madola (Ghana, Nigeria, n.k.) kuwaleta Britain kuwapa mafunzo mafupi kwenye British medical universities ili kuwapatia kazi around UK kuziba pengo kubwa lililoko. 

Doctors wanaosoma hapa Britain toka nchi za Africa wengi wamesha ahidiwa vituo vya kazi na malipo mazuri wabakie Britain.

Comment by CHA the Optimist on June 30, 2012 at 18:51
Serikali ya sasa ina uwenda wazimu. Kila daktari anagharamiwa pesa nyingi sana kumsomesha, na kumsomesha daktari mmoja inachukua miaka si chini ya mitano--kwa hiyo ukipiga hesabu hapo utaona ni jinsi gani ambavyo serikali hii inavyofanya maamuzi kana kwamba wafanyao maamuzi hayo wana itilafu katika ubongo wao. Kifupi ni kwamba nchi imemshinda huyu kiongozi wa sasa ndio maana misafara yake siku zote inashambuliwa na mawe.
Comment by Mama Malaika on June 29, 2012 at 20:13

Nchi za wenzao hawafukuzi doctors kirahisi kisa aliandamana akidai haki yake. Ndio maana wabongo wengi walio west wakimaliza kusomea medicine hawarudi TZ, sirikali za west zinajua sana kuthamini mchango wa taaluma hii na sio TZ.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*