Tulonge

Madam Ritha akanusha uvumi wa yeye kumshitaki Ney wa Mitego

Ney wa Mitego kushoto, na Madam Ritha

Mkurugenzi wa Benchmark Productions Limited, ambao ndio waandaaji wa EBSS Madam Ritha Poulsen amekanusha habari ya kumpandisha kizimbani mwanamuziki wa Bongo fleva Ney wa Mitego kwa kosa la kumsema Ritha kuwa hawapatii hela washindi wa BSS(Bongo Star Search) pamoja na maneno mengine ambayo yapo kwenye wimbo wa Salaam zao wa mwanamuziki huyo.Pia ilisemekana angemdai fidia ya Tsh. mil 500 kwaajili ya kumdhalilisha

 

Akizungumza na Clouds Fm, Ritha alisema hana mpango wa kumshitaki msanii huyo kwani hana muda wa kufanya jambo hilo. Hata hivyo Ney hana uwezo wa kulipa fedha hiyo. Muda kwake ni mali hivyo hawezi kuupoteza kwa jambo hilo. Alipoulizwa kama anaweza kumruhusu Ney aje kuimba kwenye fainali za EBSS za mwaka huu, Ritha alijibu anaweza kabisa kumruhusu na atapenda aimbe wimbo huo huo wa Salam zao.

 

Aliongeza kwa kusema Ney atakua ametumia fursa hiyo ili kujulikana zaidi kwa watu, na ni kweli amefanikiwa sababu hata yeye (Ritha) amemjua vizuri.

 

Katika wimbo wa Salaam zao, Ney alimponda mshindi wa EBSS 2012 Walter Chilambo kuwa ana maisha magumu japo alitangazwa kushinda mil 50. Kutokana na hili Ney alihitimisha kwa kudai hela za washindi wa BSS huwa haziwafikii walengwa.

 

Pia katika wimbo huo amegusia watu mbalimbali maarufu wakiwemo Rais, wabunge, wanasiasa na watu wengine maarufu.

 

Sikiliza hapa wimbo wa Salaam zao

Views: 690

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on August 26, 2013 at 15:44

Hahahahaaaaa.... EEE wacha amwambie Dingi yake masela hawamuelewi kabisa... hahahaaa

Comment by Tulonge on August 24, 2013 at 23:01

Duuh!Ney chizi aisee! yani haogopi wala nini. Eti Ridhiwan mwambie dingi yako masela hawamuelewi.........

Comment by ANGELA JULIUS on August 24, 2013 at 9:26

HUYU MAMA NDO MAANA ANAZIDI KUFANIKIWA HANA MUDA MCHAFU NA WACHAFU. NEY MTOTO MDOGO SANA KWAKE KIUMRI HADI KIFEDHA NA NINAVOMJUA HUYU MAMA ALIVO NA ROHO NZURI KWELI ANAWEZA KUMWALIKA AJE AIMBE KWENYE EBSS.

HAPA AMENIFUNDISHA KITU USILIPE UBAYA KWA UBAYA BALI USHINDE UBAYA KWA WEMA.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*