Tulonge

Magufuli asisitiza kutobadilika kwa nauli mpya za vivuko vya kigamboni licha ya wananchi kutoridhishwa na suala hilo.

Waziri wa Ujenzi  Dk John Magufuli amesisitiza kuwa serikali haitabadilisha kamwe nauli mpya ya vivuko vya kigamboni kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji kama mafuta na mishahara ya wafanya kazi wa vivuko hivyo. Pia vivuko vya kigamboni ndivyo vivuko pekee vyenye nauli ya chini ukilinganisha na nauli za vivuko vingine vingi  hapa nchini.

Aliongeza kuwa wananchi wamekuwa wagumu kuelewa kuwa nauli za awali zilianza kutumika tangu miaka 14 iliyopita huku kukiwa na kupanda kwa gharama za uendeshaji lakini serikali haikupandisha nauli. Chakushangaza sasa wananchi wanakuja juu baada ya kupandishiwa nauli wakati serikali iliwavumilia kwa kipindi kirefu sana bila kupandisha nauli.

Amesisitiza kuwa wananchi watakao amua kuandamana watatozwa nauli mpya endapo wanapanda kivuko wakati wa maandamano yao. Wasidhani watatozwa nauli za kawaida kwa kuwa wanaandamana.

Magufuli alimaliza kwa kuahidi kuwa wataweka mifumo ya kieletroniki ili kudhibiti mapato ya vivuko.

**Haikueleweka ni mifumo gani ya kieletroniki itawekwa maana serikali ilishajaribu kuweka mifumo hiyo lakini ilishindikana kuitumia baada ya kuwa na mapungufu mengi. Hadi sasa kuna  mabaki ya mifumo hiyo ambayo haitumiki.**

Views: 266

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on January 7, 2012 at 14:32

Ndo viongizi wetu hao, tuliwachagua wenyewe, tunateseka wenyewe

Comment by Tulonge on January 3, 2012 at 0:32

Huyu Magufuli anavyosifiwa kuwa anafanya kazi vizuri basi naona analewa sifa na kuanza kuongea ishu zisizo za kawaida. Sikutegemea mtu kama huyu anaweza waambia wananchi wa Kigamboni waogelee endapo watashindwa kulipa nauli. Halafu yeye anajiona kaongea pointi kweli. Kwahiyo na kina mama wajawazito, wazee,vilema wote waogelee kama hawa nauli?

Comment by CHA the Optimist on January 2, 2012 at 20:58
Hatutaheshimiana mpaka hapo siku tutakaposhikana mashati na kutwangana makonde. Maana hawa jamaa wanafikiri sisi ni vidudu mtu. Kauli zaokwanza za kipuuzi, yaani sisiti kuwafananisha na wahuni.
Kila siku wanazidi kumpandishia mwananchi gharama za maisha, wao wanazidikujipunguzia mzigo wa maisha kwa kutaka kupeana posho za laki mbili kwa siku. Pumbavu! Nimemsikia huyu Magufuli ambaye baadhi ya watu humsifu kwa uchapa kazi--akisema gharama za uendeshaji zimepanda kwa maana ya mafuta na vitu kama hivyo. lakini swala la kijiuliza hapa ni kwamba--hivi kila mwananchi hutumia lita yake ya mafuta anapoingia kwenye chombo cha usafiri? Nimechoka kwa kweli na hii nchi yenye viongozi uchwara kama hawa akina magufuli na bosi wake. Ipo siku nasema.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*