Tulonge

Makosa ya Godbless Lema(CHADEMA) VS Makosa ya Livingstone Lusinde(CCM)

Nimeona nije kuliweka mezani suala hili la makosa aliyofanya Lema na Lusinde(Mbunge wa Mtera) katika Kampeni za Ubunge japo ni katika vipindi tofauti. Wazo hili nimelipata baada hukumu ya Lema kutoka ambayo ni kumfuta ubunge na kumkataza kugombea ubunge kwa kipindi kisichopungua miaka mitano.

Jaji Gabriel Rwakibarila alimtia hatiani Lema kwa makosa mawili kati ya manne aliyokuwa akikabiliwa nayo.

Makosa hayo ya Lema ni:-

1. Lema alitiwa hatiani kwa kudaiwa kusema kuwa Dk Burian hakustahili kuchaguliwa kuwa mbunge kwa sababu mila na desturi za makabila ya Waarusha (Wamaasai na Wachaga), mwanamke hawezi kuongoza wazee.

2. Sababu ya pili aliyotumia Jaji kutengua ubunge wa Lema kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Dk Burian kuwa ni mwanamke asiye mwaminifu, aliyezaa nje ya ndoa na alikuwa na mimba nyingine na bwana huyo aliyezaa naye ambaye siyo mumewe.

Jaribu kuorodhoshe makosa ya Lusinde kupitia Video hii:-

Umegundua kuwa Lusinde anamakosa yanayoendana na yale ya Lema? Je Lusinde ATAFUTWA ubunge??

Views: 1023

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on April 9, 2012 at 11:07

kuna msemo "nyani haoni kundule" ...

Comment by Tulonge on April 7, 2012 at 16:50

Hahahahahahhaaa Mama M umenifurahisha japo inasikitisha kwa upande mwingine. Kwahiyo amemzalilisha na mama na bibi yake bila kujijua???

Comment by Mama Malaika on April 7, 2012 at 14:58

DISMAS nakwambia huyo Lusinde wakisema kila mtu anayehisi amekwaza amshtaki basi hata mie pia nitamshtaki kwa kauli yake ile ya "mwanamke mwenye mimba". Kauli hiyo imedhalilisha wanawake wote akiwemo mama yake mzazi na hata bibi zake.

Comment by Mama Malaika on April 7, 2012 at 14:29

kaka Eddie bora useme wewe, huyu bwana hapa kwetu angeipata.

Kwa nyie mlioko Tanzania mnaelewa ukweli kuhusu makosa  ya huyo kijana Lema aliyehukumiwa. IWAPO ni kweli alisema kauli ya hilo tamko kwenye kosa la kwanza alilohukumiwa anafanya kosa kwani gender discrimination. Unapokuwa kwenye jukwaa la siasa hutakiwi kuongelea sera ambazo zinakandamiza kundi la watu fulani kwenye society hasa kipindi ambacho Tanzania inajitahidi kufuta ubaguzi dhidi ya makundi fulani iwe ya kijinsia au kidini.

Comment by CHA the Optimist on April 7, 2012 at 12:09

Nimeshindwa kusikia maneno yake kwa sabu sina speaker, hivyo siwezi kutoa maoni.

Comment by eddie on April 7, 2012 at 10:44

Huyu angekuwa ughaibuni angekuwa ndani.

Comment by Stephen Minja on April 7, 2012 at 10:34

Huyu Bwana hatujui eee

 

Comment by manka on April 7, 2012 at 6:15

HUYU SIKU ZAKE ZINAHESABIKA ZA KUITWA MHSHIMIWA, MAANA HATA HAITAJI KUPELEKWA MAHAKAMANI.

Comment by Tulonge on April 6, 2012 at 22:45

Hahahaaa hapo kwa Lusinde unaweza ukagundua makosa mengi sana. Maana kila aliyetukanwa akisema amshitaki itakua balaa. Atashitakiwa na Lema,Mbowe,Slaa halafu atashitakiwa na Chama cha Chadema. Bado ishu ya kuwadhalilisha wanawake kwa kuizungumzia mimba vibaya,na mengine kibao.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*