Tulonge

Mama amchoma mwanae kwa mkasi mara 90 kwa madai ya kumng'ata alipokua akimnyonyesha

Ni kama miujiza kwa mtoto wa kichina kuwa hai mpaka sasa licha ya kuchomwa chomwa mara 90 na mama yake mzazi huko China kwa madai kuwa alimng’ata ziwa mama yake wakati akinyonyesKwa mujibu wa Daily Mail mtoto huyo Xiao Bao mwenye miezi 8 tu ameshonwa zaidi ya nyuzi 100 ili kuurudisha uso wake katika hali nzuri baada ya shambulizi hilo lililotokea katika jiji la Xuzhou mashariki mwa China.

Bao anaishi na mama yake pamoja na wajomba zake wawili ambao wanajishughulisha na ukusanyaji wa taka kwaajili ya kipato. Mmoja wa wajomba hao ndiye aliyegundua kuwa Bao ameumizwa baada ya kumkuta akiwa amelala kwenye damu iliyotapakaa nyumbani hapo kabla hajamkimbiza hospitali.
Mama wa mtoto huyo baadaye alikiri kumchoma choma mwanae na mkasi mara 90 hususan eneo la usoni baada ya mtoto huyo kumng’ata ziwa wakati akimnyonyesha.

Baada ya tukio hilo majirani wa familia hiyo wameiomba serikali imnyang’anye mama huyo wa kichina mtoto kwa sababu za kiusalama, lakini ombi hilo limekataliwa kwa madai kuwa hakuna uthibitisho wowote mpaka sasa kama mwanamke huyo anamatatizo ya akili, lakini wameongeza kuwa hata hivyo mtoto huyo bado ana walezi wengine wawili anaoishi nao (wajomba zake) Mtoto huyo anaendelea kupata nafuu akiwa hospitali.

Via: Audiface Jackson Blog

Views: 914

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Holiness Bangereza on July 25, 2013 at 22:10
Duuh that woman anaroho ya kishetani zaidi ya shetani mwenyewe
Comment by manka on July 22, 2013 at 12:59

mhuuuu!!

Comment by salum kitila on July 21, 2013 at 15:47

mmh

Comment by Christer on July 18, 2013 at 12:50

Kichaa huyo mama, kweli achunguzwe akili.

Comment by sakina mgaya on July 15, 2013 at 22:30

mhhh kama ni kweli bas huyo mama achunguzwe lazima ana matatizo ya akili sio bure

Comment by Dixon Kaishozi on July 15, 2013 at 10:55

Dah!!!! najiuliza kale kamsemo kama kana ukweli juu ya hili.... Uchungu wa mwana aujuae ni MZAZI... 

Comment by SHARIFA MKUMBARU on July 13, 2013 at 15:06

Kiukweli huyo  mwanamke ana roho ya kikatili sana,  anastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*