Tulonge

Waziri wa Elimu Phlip Mulugo

*Nusu ya wanafunzi wafeli vibaya, wasichana safi
*Shule 10 za mwisho zatoka Lindi, Mtwara
MATOKEO ya mtihani kidato cha pili uliofanyika mwaka jana, yametangazwa jana na kuonyesha karibu nusu ya watahiniwa wakifeli mtihani huo. Akitangaza matokeo hayo mjini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema jumla ya wanafunzi 249,325 kati ya 386,271 waliosajiliwa wamefaulu, ambao ni sawa na asilimia 64.5.

Alisema licha ya ufaulu kuongezeka kutoka asilimia 44.4 mwaka 2011, hadi 64.5 mwaka jana, wanafunzi 136,923 sawa na asilimia 35.45 hawakufaulu mtihani huo.

Alisema wanafunzi hao, wameshindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tatu kutokana na kutofikia asilimia 30 za ufaulu zilizopangwa na Serikali.

Alisema kati ya wanafunzi 136,923 walioshindwa kufaulu, wasichana ni 74,020 na wavulana 62,903 ambao wamepewa fursa tena ya kurudia darasa.

Alisema katika matokeo hayo, wanafunzi wote 10 bora wametoka shule mbili za binafsi, huku shule za Serikali zikionekana kufanya vibaya.

“Wanafunzi waliofaulu ni 249,325, kati yao wasichana ni 113,213 na wavulana 136,112, kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 19.15 kutoka 45.40 mwaka 2011.

“Watahiniwa waliofaulu kwa alama A, B na C ni, 127,981 sawa na asilimia 33.13 na waliofaulu kwa alama D ni 121,344 sawa na asilimia 31 ambapo alama ya juu ya ufaulu ni asilimia 92.

“Idadi ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani mwaka jana, walikuwa 430,327, kati yao wasichana walikuwa 205,476 sawa na asilimia 7.76, ikilinganishwa na mwaka 2011, ambapo walikuwa 466,567, watahiniwa 44,o56 sawa na asilimia 10 hawakufanya mtihani na kati ya hao wasichana ni 18,231 na wavulana ni 25,825.

“Sababu za kutofanya mtihani huu ni utoro, kuugua, kudaiwa ada, kufukuzwa shule, mimba na vifo,” alisema.

WANAFUNZI 10 BORA

Katika hali ya kushangaza, maofisa wa wizara hiyo wamezuia kutangaza au kuandika majina ya wanafunzi 10 bora kitaifa, kwa madai kuwa kuna kasoro ya kiufundi.

Alisema katika mtihani wa mwaka huu, wasichana wameongoza ambapo kati ya 10 bora wameshika nafasi saba, huku tatu zikichukuliwa na wavulana.

SHULE 10 BORA

Waziri Mulugo, alizitaja shule za Serikali zilizoshika nafasi 10 za mwanzo kuwa ni Mzumbe, Tabora Wavulana, Ilboru, Kibaha, Iyunga, Msalato, Malangali, Ifunda Ufundi, Samora Machel na Kilakala.

SHULE BINAFSI

Kwa upande wa shule za binafsi katika nafasi hizo 10 bora ni, Kaizirege, Marian Wavulana, St. Francis, Don Bosco, Bethel Sabs, Marian Wasichana, Canossa, St. Joseph Iterambogo Seminari na Carmel.

SHULE 10 ZA MWISHO

Mulugo alisema ameshangazwa na hali ya shule za Serikali zilizoshika nafasi 10 za mwisho, zote kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi.

Mulugo alizitaja shule hizo ni Mihambwe, Dinduma, Kiromba, Marambo, Mbembaleo, Kinjumbi, Litupu, Luagala, Miguruwe na Napacho.

SHULE 10 BINAFSI ZA MWISHO

Vile vile alizitaja shule za binafsi zilizoshika nafasi 10 za mwisho ni Mfuru, Pwani, Doreta, Kigurunyembe, Kiruma, At-taaun, Jabal Hira Sem, Mkono wa Mara, Kilepile na Kiuma.

Alisema Serikali, haitakuwa na huruma kwa wazazi watakaowazuia wanafunzi kutokariri kidato cha pili mwaka huu, kwa sababu ya kuwaoza au kuoa.

“Kumekuwa na tabia ya wazazi kuona mwanafunzi ameshindwa kufaulu na kutumia mwanya huo kuwaoza, sasa nasema hilo nitalifuatilia kwa ukaribu kwa kushirikiana na ngazi ya mkoa, wilaya na tarafa, ili kuwabaini na kuwachukulia hatua.

“Naombeni wazazi wawe na tabia ya kufuatilia maendeleo ya watoto na kukaa nao siku za mapumziko ya wiki na kukagua daftari zao, suala la elimu lisiachwe kwa walimu pekee, hii ndio inasababisha hata shule 10 zote za mwisho zinatoka kanda moja.

AJIRA

Mulugo amesema wizara haijapanga kutoa ajira kwa walimu wote waliopo katika manispaa kufundisha mjini, kwa lengo la kupunguza tatizo la upungufu wa waalimu maeneo ya vijijini.

Alisema walimu wengi waliopo mjini, hawapendi kupangiwa kufanya kazi vijijini, hali inayopelekea kuwa na ongezeko kubwa la ukosefu wa waalimu, Serikali kwa makusudi imeamua kutotoa ajira kwa walimu mpaka idadi ya uwiano wa walimu itakapokuwa sawa.

Alisema mpango wa Serikali, utakuwa endelevu hadi itakapofikia mwalimu mmoja kusomesha wanafunzi 40 katika darasa.

Alisema idadi ya shule za sekondari imeongezeka kutoka 971 hadi kufikia 4,528, hii inaleta hamasa katika wizara ya elimu kwani kunaongezeko kubwa la wanafunzi shuleni.

“Asilimia 70 ya fedha hizi, zitapelekwa katika bodi ya mikopo kwa ajili ya kupatiwa wanafunzi wa vyuo ila kwa kufuata utaratibu uliopangwa,” alisema Mulugo.

Alisema wanafunzi wa vyuo vikuu, walijitoa katika uwanafunzi na kuhamia katika siasa hali iliyopelekea mgomo na mgogoro kwa baadhi ya vyuo vikuu kwa madai ya kutopatiwa mkopo.

Habari hii, imeandaliwa na Benjamin Masese, Hadia Khamis na Yoachim Ndimbo.

Chanzo: mtanzania.co.tz

Views: 1520

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on January 13, 2013 at 8:17

Mama hilo usemalo pia lipo.Ila hawa madogo wa siku hizi nao ni wazembe sana. Hata sisi tulisoma katika mazingira hayo hayo ya kutokua na vitabuna vifaa vingine vya practical lakini tulikua tunajitahidi. Mwalimu alikua anatuandalia notes toka kwenye kitabu chake halafu sisi tunakomaa na hizo notes hadi kieleweke.

Kuna baadhi ya shule utakuta wana kila kitu ila matoto yanachemka vile vile.Hawa wa sasa starehe zimewazidi sana.

Comment by Severin on January 13, 2013 at 6:59

Pia watoto wa siku hizi wamezidi kungonoka

Comment by Mama Malaika on January 12, 2013 at 23:04

Mashuleni vitendea kazi ni haba, hapo usitegemee matokeo yakawa mazuri. Nimetembelea shule 13 na zote hawana vitabu vya wanafunzi na maabara zao Mungu mwenyewe ndiye anayejua. Na tatizo unawapatia walimu vitabu ajili ya kuwapatia wanafunzi, unarudi mwakani hukuti hata kimoja

Comment by Tulonge on January 12, 2013 at 21:36

Enzi zetu tukiwa form 2 hata TV zilikua za kutafuta.Hiyo computer kuiona ilikua shughuli,hukuti mwanafunzi anamiliki simu. Nadhani hivi vyote ni changamoto kwa watoto wa kizazi hiki. Kwahiyo inabidi wajifunze kukabiliana navyo.

Comment by Masha waryoba on January 12, 2013 at 15:19
Hayo matokeo ni lazima yawe hivyo,ttz liko pande zote!serikali haiko serious,walimu ndo usiseme,wazazi wenyewe hawako commited kwa watoto wao,ukija kwa wanafunzi wenyewe ndo basi!!wako busy na mtandao wa kijamii!tunajenga taifa gani!!?
Comment by Tulonge on January 12, 2013 at 14:54

Weweweeeeee nimefurahi kuona Shule yangu Malangali bado ipo juu Kitaifa, naona madogo bado wanaendeleza kufuata nyayo za kaka zao.

Ila kwa ujumla matokeo haya yanasikitisha.Sijajua kama ni huku kukua kwa teknolojia ndo kuna waponza. Wanashindwa kuitumia teknolojia vzr.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*