Tulonge

Membe "Mliopo mikoani msije Dar hadi Obama atakapo maliza ziara yake"

Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe(PICHANI) amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.

 

Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.

 

“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.

 

Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.

 

“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”

 

Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.

 

Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.

 

Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na wakati huo.

Views: 528

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Monica Male on June 28, 2013 at 15:53

Jamani tusipotoshane hapa barabara zitafungwa muda ule tuu wanaopita na wala haizidi nusu saa.

Pia airport itafungwa for one hour only nusu saa kabla ya kufika na nusu saa baada.

Mkuu wa mkoa ameshatolea maelezo yote hayo jana ITV. Watu tusiahirishe shughuli zetu kwa kisingizio cha ujio wa Obam

Comment by Mama Malaika on June 28, 2013 at 15:25
Mgao Siamini.... Nami nakuunga mkono, kuabudu watu kunarudisha mambo nyuma. Wenzetu hawaendekezi ujinga wa kuabudu. Nilikuwa TZ for few days, nimeshukuru kuondoka kabla ya Obama maana ndege yake tayari imevuruga timetable ya airlines zinazotua JK Nyerere Airport siku hiyo anapowasili na siku ya kuondoka. Hapo revenue yapungua (aircaft parking charges, etc.) na kwa wengine tunaosafiri kikazi inakuwa shida sana hiyo siku, na wasafiri wagonjwa ndio nawaonea huruma sana
Comment by Mama Malaika on June 28, 2013 at 15:11
Hata kama barabara chache yapaswa ifungwe kwa saa moja tu na sio masaa. Na ile tabia ya viongozi wa chama na sirikali wote na magari yao kulundikana Airport ndio inayoleta kero. Kama nilivyosema, UK wanatuma gari moja tu toka Downing Street no. 10 kupokea mgeni na pia pikipiki za usalama ni chache sana. Barabara ya inner city kuingia kwa waziri mkuu, jengo la bunge au kwa Malkia ni ile ile tupitayo watu na hukuti inafungwa zaidi ya saa moja. Na hata kiongozi David Cameroun anapokuwa ziarani huwezi jua kwani msafara ni gari 2 tu. Tanzania raisi tu ile kwenda Bagamoyo safari yake binafsi kuona nduguze weekend wakuta ni msululu wa magari ya sirikali sijui FFU, zima moto, ambulance, etc. pesa ya walipa kodi inamalizikia mafuta ya magari misafara.
Comment by MGAO SIAMINI,P on June 28, 2013 at 12:46

si wa Iringa hatuna haki ya kumuona obama live,sasa kama tunaumwa au tunataka huduma maana unajua hata gesi ya mtwara inaenda huko itakuaje? jamani tuache kuabudu watu mambo yaendelee mtazamo wangu.

Comment by KUNAMBI Jr on June 28, 2013 at 9:00

kwa nilivyomuelewa Membe nahisi yuko sahihi,hajasema kwamba watu wasije Dar ila yeye katoa ushauri kutokana na kero watakazozipata tu

Comment by Monica Male on June 27, 2013 at 15:03

Mama Malaika ni sawa unavyosema lakini ukumbuke huku nyumbani barabara zetu ni chache kama ile yakutoka airport ni moja tuu kwa hiyo kufungwa ni lazima. Huwezi kulingamisha na huko kwenye barabara za juu na chini na trani pia.

Pili hatuna mahoteli mengi kama huko London unakosema ndio maana wageni wameombwa wasije kutoka mikoani kwani watapata shida ya mahali pa kukaa.

Tatu airport  yetu ni moja tuu hatuna nyingine hapa dar kama hizo ulizotaja huko uliko hivyo kwa usalama wao pia ni budi zifungwe kwa muda huo waliosema kwa usalama wa wageni wetu.

Umaskini wetu wa kukosa miundombinu ya kutosha ndio imepelekea hayo yote, kwahiyo wnanchi wa Dar tusilalamike sana tuvumilie kwa hizo siku chache.

Comment by Mama Malaika on June 27, 2013 at 12:16
Site weusi tunapenda sana kukuza mambo, sijui ni ujinga auukarimu ndio unatuponza? Na hao ni viongozi 11 tu na wake zao wajao Tanzania, haya iwapo ingekuwa world summit yafanyika jiji la Dar na Malkia naye aja si ndio ingekuwa balaa kwa wananchi wa Tanzania? Na wajawazito wa Dar wanaotegemea kukifungua hiyo siku naona wengi watajifungulia majumban, au wagonjwa wanao hitaji kwenda Hospitals zilizo Dar nawaonea huruma sana. Nchi za west hukuti wenyeji wanakoseshwa raha eti ujio wa wageni.... Wazungu hawana ukarimu huo na hizo misafara ya foleni kupokea wageni kwa sirikali zao haiko kwani hawana magari wala muda wa kuchezea. Akili yao ni kubana matumizi tu ndio maana wakuta mawaziri wa UK hawako entitled kuwa na gari ya office zaidi ya ku panda train or private car.
London kulifanyika World Summit mwaka juzi, Obama na wenzie hawakutukosesha usingizi na watu tulisafiri kwenda London kama kawaida ukizingatia wengi asubuhi twaenda London kufanya kazi na jioni kurudi mikoani majumbani by cars or trains. Na hizo ndege zao sijui Airforce one ziliambiwa kutua kwenye small airports za London (Stanstead, Luton & London city airport) na sio London's world leading international airports (Heathrow and Gatwick) kuvuruga timetable ya wasafiri.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*