Tulonge

Miss World 2013: Hakutakuwa na vazi la bikini katika shindano la kumsaka mrembo wa dunia mwaka huu!

Shindano la kumtafuta mrembo wa dunia kwa mwaka huu 2013 linategemewa kufanyika huko Indonesia, lakini utofauti utakaokuwepo ni kwamba washiriki hawatavaa vazi la bikini kama ilivyozoeleka katika mashindano yaliyopita.

Kwa mujibu wa mtandao wa aceshowbiz waandaaji wa shindano hilo la mrembo wa dunia 2013 wametoa taarifa ya uamuzi huo Jumanne wiki hii (June 5) ikiwa ni hatua ya kuepukana na kutofautiana na vikundi vya kiislam vya Indonesia ambayo aslilimia 90 ya wananchi wake ni waislam.

Msemaji wa RCTI waandaaji rasmi wa Miss World 2013 nchini Indonesia, Adjie S. Soeratmadjie alisema
“Kutakuwa hakuna bikini katika shindano la miss world mwaka huu ili kuheshimu mila zetu za jadi na maadili, Hili ni suala nyeti hapa Indonesia.. Tumejadiliana tangu mwaka jana na wamekubali.”

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika mwezi september mwaka huu (2013).

Chanzo: Bongo5

Views: 320

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on June 8, 2013 at 6:55

-Vp kuhusu hayo mapaja na matumbo yaliyo wazi? Hivyo vikundi vya Kiislam vimekubaliana na hilo?

-Kwanza kwa nini haya mashindano huwa yanasimamishwa endapo yakiangukia kwenye mwezi  Mtukufu? Mbona mashindano mengine kama football nk huwa yanaendelea hata kama ni Mwezi Mtukufu?

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*