Kesi za unyanyasaji dhidi ya wanawake zinazidi kuwa nyingi. Wanawake
wameendela kuumizwa na ubabe wa waume zao. Hivi karibuni, katika kijiji cha
Kizanda wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa
jina la Bi. Rahima alifariki dunia baada ya kupigwa na mumewe mateke ya
tumboni angali mja mzito.
Taarifa za awali kutolewa zinasema kuwa mwanamke huyo alifariki kutokana na
homa, lakini ndugu wa marehemu wamedai kuwa kifo cha ndugu yao kimetokana
na kipigo. Bi Rahima ambaye alikuwa ni mja mzito, alifariki mwezi wa saba
mwaka huu.
Taarifa za awali ambazo zilifikia Wanawake Live na Super Woman Joyce Kiria
kufuatilia zilionekana kupita EATV usiku wa jana, na pia unaweza kufuatilia
kwenye YouTube kupitia linki hii hapa chini ili ufahamu kile wanasheria
wamekizungumza katika kutafuta haki kufuatia suala hili ambalo hata
viongozi wa kijiji hicho wameshindwa kulitatua.
Via: othmanmichuzi.blogspot.com
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge