TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) imesema mkoa wa Njombe unaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya UKIMWI kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1.
Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya nne kwa asilimia tisa ukifuatiwa na Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Msemaji wa TACAIDS, Glory Mziray alisema hayo jana Dar es Salaam na wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mikoa mingine na viwango vyake ni Mara (4.5), Mwanza (4.2),Mtwara (4.10), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).
Alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya UKIMWI yamepungua kwa kasi ndogo.
Alisema watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya ukimwi na UKIMWI wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.
Kuhusu tohara kwa wanaume endapo inapunguza maambukizi ya UKIMWI alisema inapunguza kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja kutoa elimu zaidi juuya uelewa wa ugonjwa huo
Via: kajunason.blogspot.com
Add a Comment
Arusha iko safe e maana sijaiona kwenye list hapa. hahahahahah huu ugonjwa kwa sisi huku nchi zisizokua na muelekeo maalumu utatumaliza huku tukijidanganya na takwimu za kwenye makaratasi maana hizo sawa ni research lakini always research hua zinatumia sample space so sample space haiwezi kugusa kila mhusika.. Tujitahidi kujikinga waliooa watulie na ndoa zao ambao hawajoa watulie na watarajiwa wao basi!! sio mara leo hapa kesho pale tutakwisha
Duuh! mama hiyo yakuwatia jela ikifanyika huku kwetu watu watasema ni unyanyapaa, japo kweli itasaidia kupunguza maambukizi. Pia kutakua na kazi kubwa sana kuwabaini wafanyao mapenzi huku wakijujia ni waathirika. Kwani hao wenzetu wa huko wanawabaini vp?
Halafu watakamatwa walala hoi tu, wenye hela zao wataendelea kusambaza virus kwa raha zao tena bila kuulizwa.
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge