Tulonge

Mmh! Huyu Mwalimu anatoa adhabu kwa wanafunzi au anaua joka?


Nimekutana na hii video sehemu ila nimeshindwa kutambua ni mwalimu wa shule ya nchi ipi. Sina hakika kama adhabu hii ni halali kutolewa kwa watoto hawa au la. Nguvu itumikayo ni balaa, utadhani anaua joka. Na watoto wake huwa anawaadhibu hivi?

Views: 1305

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Gratious Kimberly on August 2, 2013 at 20:42

Duh....noma kama sio maigizo basi hii ni balaaa.   Mimi kwa harakaharaka  nimeona hapo ni Shule nchini Kenya....pale anapopiga kiboko cha kwanza anaogea lugha ya kiswahili cha Kenya akisema.." Nilisema nini"?

Comment by Mama Malaika on July 27, 2013 at 10:59
Mgao Siamini.... ualimu ni kazi ngumu sana na ni professional muhimu sana kuandaa taifa la kesho, ndio maana wenzetu mwalimu ana thaminika na mshahara wake unatosha kukidhi mahitaji ya lazima.

Huyu mwalimu akifundisha shule wanayosoma wanangu naona atafungwa jela miaka 100+ na kuvuliwa membership ya ualimu. Hata mie mzazi sirihusiwi kumpa mtoto adhabu hii. Wataalamu wanatuambia adhabu hizi zampa makovu mtoto (psychologically) ya kudumu. Mental and emotional state tunayokulia mazingira ya utotoni ndio hiyo yazaa tabia zetu ukubwani. Ukatili ndio source kubwa ya controlling behaviour, lack of confidence & self-esteem.
Comment by jemadari mimi on July 25, 2013 at 14:05

Kwa kweli c busara kwa mwalimu ama mzazi kutumia nguvu kupita kiasi kwa kumdhibiti mtoto au kijana wako, tunajua kuwa vijana wetu hawa wasomi wa leo wana matatizo sana ya dharau,kiburi na kujiona wanajua mambo zaidi ya walimu ama mlezi wake.

Mwalimu kama mwalimu ana wajibu wakurekebisha tabia ya mwanafunzi wake pale anapoona hayuko sawa kitaaruma na kimaadili.lkn adhabu ambazo walimu wanazitoa mara nyingi ni kubwa kuliko kosa lenyewe,muda mwingine walimu na mwanafunzi uchapana makonde.

Comment by MGAO SIAMINI,P on July 16, 2013 at 18:30

ATAKUA ANASTRESS ZA MSHAHARA MDOGO MAANA WALIMU AFRIKA WANALIPWA KIDOGO,HAWAHESHIMIWI HALAFU KATIKATI YA MWEZI PESA KALIPA MADENI HALAFU WATOTO WANAZINGUA ATAUA.

Comment by SHARIFA MKUMBARU on July 16, 2013 at 13:22

Duuuuh! kweli hii kali mwalimu,  "maana ticha  anavyowachapa wanafunzi kama vile anaua nyoka". Tabia hii inayofanywa kwa baadhi ya walimu si njema na wanastahili wapewe onyo kali.

Comment by jacquerin gideon makoyola on July 16, 2013 at 11:40

Hiii ni balaa

Comment by Tulonge on July 16, 2013 at 9:45

Inaonekana kuna mwanafunzi alikua na cm yenye camera ndo aka-mrekodi. Angestukiwa angelijua jiji, hasira zote zingemuishia yeye

Comment by Dixon Kaishozi on July 16, 2013 at 9:29
Hahaaaaa... kama konda wa daladala walivyozoea kuning'inia mlangoni matokeo yake wanajazia upande.. hahaaa
Comment by Tulonge on July 16, 2013 at 9:05

Yani anatumia nguvu nyingi sana.Akiendelea hivi kwa miezi miwili atajazia mkono wa kulia kuliko wa kushoto

Comment by Dixon Kaishozi on July 16, 2013 at 8:50
Huyu nae anafaa achapwe kwa staili hiyo hiyo aone utamu wake.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*