Tulonge

Mpeleke mwanao akapate mtone ya Vitamin A,zimebaki siku 4 tu kwa awamu hii.


Wadau nimeona tukumbushane juu ya hili suala la kupeleka watoto wetu wakapate huduma ya BURE ya matone ya Vitamin A na Dawa ya minyoo inayotolewa kwenye vituo mbali mbali vya afya. Matone ya Vitamin A ni kinga dhidi ya magonjwa kwa mtoto wako. Huduma hii imeletwa kwenu na Wizara ya Afya na ustawi wa jamii, ambayo hutolewa mara mbili kwa mwaka yaani mwezi wa 6 na mwezi wa 12. Zimebaki siku nne tu zoezi kukamilika kwa awamu hii. Ukikosa utalazimika kusubiri hadi mwezi wa 12.

Matone hayo hutolewa kwa mtoto wenye umri kati ya miezi 6 hadi miaka 5. Si lazima mtoto apelekwa na mama, hata akina baba tunaweza peleka watoto. Ni zoezi la dakika chache tu, hakuna kupoteza muda. Mpeleke mwanao kituo cha afya kilicho karibu yako apate huduma hii.

Nafahamu Watanzania tulivyo na tabia ya kupuuzia vitu.

Views: 308

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on June 29, 2012 at 5:07

Asante kwa ushauri mama Malaika

Comment by ALFRED ADOLF MWAKAPESA on June 27, 2012 at 16:47

Thanx our rafiki

Comment by Mama Malaika on June 27, 2012 at 13:13

Mie kama mama mzazi hiyo Vitamin A liquid drop ndio leo naisikia. Hapa tuna liquid drops za Vitamin B & D. Na watoto wetu pindi wamalizapo chanjo na matone ya uchanga miezi 3 ya kuzaliwa hawapewi tena matone. Tunasisitizwa kuwapa vyakula vyenye source ya hizo vitamins ku boost immune system.

Kutokana na hali ya hewa nchi zetu za tropical kuwa joto, pia umeme kukatika kila wakati, nina mashaka makubwa na hiyo Vitamin A inayotolewa kwa watoto kwani storage ya liquid drops inatakiwa kuwa baridi muda wote. 

 

Mie kama mama mzazi, ninashauri wazazi wenzangu kuwapa watoto wenu vyakula yenye hiyo Vitamin A. Matunda, maboga, na mboga mboga za majani Tanzania ni nyingi sana tena tena ziko fresh. Tunda la ndizi na carrots ni source kubwa sana ya Vitamin A, mpe mwanao kila siku ukiweza ku-boost immune system ya mtoto wako.

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*