Tulonge

Mrisho Mpoto awaomba wezi wamrudishie vifaa vya gari lake walivyo muibia

Msanii wa miondoko ya kughani Tanzania Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ amewaomba wezi waliomuibia vifaa vya gari lake siku chache zilizopita wamrudishie. Akiongea kwa njia ya simu na Clouds FM Radio, Mjomba alisema yupo tayari kuvinunua vifaa hivyo kwa sh. Mil 2 endapo wezi hao watamrudishia. Kwa mujibu wa Mjomba, vifaa vilivyoibwa vina thamani ya sh. Mil 4 kwa makisio.

Pamoja na vifaa hivyo, pia Mjomba aliibiwa ‘wallet’ yake iliyokua na hela, vitambulisho na kadi za benki. Pia aliibiwa vitabu mbalimbali vilivyokua kwenye gari.

Mjomba aliongeza kuwa angeweza kuibiwa vifaa zaidi ya vilivyoibwa endapo wezi hao wasinge kurupushwa. Hadi sasa hakuna aliyekamatwa kutokana na tukio hilo, ila ameshatoa taarifa kituo cha polisi na wameahidi kuendelea na uchunguzi.

Views: 577

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on October 27, 2013 at 17:19

Pole anko

Comment by Chikira Chikira on October 19, 2013 at 15:49

Pole sana Mjomba, wezi ni wanyama waliovaa tu ngozi na sura za binadamu, lakini wao hawana ubinadamu hata chembe!!! nawachukia sana wezi!! Mungu ata kuonyesha njia ya kupata namna ya kurudishia vifaa vyako kwenye gari lako, usikate tamaa!!

Comment by Mama Malaika on October 18, 2013 at 16:42
Pole sana. Wezi hawana utu ndio maana wanachomwa moto.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*