Tulonge

Mtihani kidato cha IV 2012:Hivi ndivyo vituko vilivyo andikwa kwenye karatasi za majibu

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako akionyesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Fredy Azzah, Joyce Mmasi
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweza kukumbwa na kashfa kubwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya 2012 yaliyotangazwa juzi na Waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa.


Kashfa hiyo inatokana na aina ya majibu yaliyoandikwa na baadhi ya watahiniwa katika mitihani hiyo, huku wengine wakikusanya vitabu vya majibu bila kujibu chochote, hali inayohusishwa na uhaba mkubwa wa walimu katika baadhi ya shule za sekondari nchini.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema wasahihishaji walikutana na mambo ya ajabu yakiwamo matusi, michoro ya vitu visivyoeleweka, mashairi na nyimbo za muziki wa kizazi kipya (bongo fleva).

“Mwaka jana tulikutana na ‘single’ yaani waliandika mashairi kwa uchache, lakini mwaka huu tumepata albamu nzima… ni vituko vitupu, wengine wanaandika mapenzi, mwanafunzi anatumia ukurasa mzima kumlalamikia mpenzi wake. Miongoni mwa yaliyoandikwa ni mpenzi, umeniacha, natamani kunywa sumu, usiku silali nakuwaza wewe…” alisema Dk Ndalichako.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Ndalichako alisema wanafunzi wengine waliandika malalamiko dhidi ya wabunge na uendeshaji wa Bunge.

“Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…” alisema.

Alisema wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka walikuwa ni wengi na walichangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya.

Dk Ndalichako alionyesha baadhi ya michoro hiyo ambayo inaonyesha vikaragosi ambavyo wanafunzi hao waliviita Messi (Lionel, mchezaji wa Barcelona) na zombi (ni picha za kutisha) ambazo huonyeshwa kwenye televisheni.

 

Soma zaidi: mwananchi.co.tz

 

Views: 896

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Hussein Nkenja on February 20, 2013 at 12:42

Usipoziba ufa utajenga ukuta; yapo mengi ya kusema ila nadhani kilichokosewa ni kuruhusu viongozi kupeleka watoto wao ktk shule binafsi na nje ya nchi. Kama watoto wa vigogo wangekuwa wanasoma ktk shule hizi basi mambo yangekuwa kama kipindi cha Mwalimu Nyerere(RIP). Yatupasa kupinga kwa nguvu na ingewezekana watu wote kuingia barabarani kupinga jambo hili na nadhani Vyama vya siasa vingekuwa vinaangalia mambo kama haya bila kujali maslahi zao binafsi. Tupambane na haya maana leo ni mtoto wa jirani kesho ni mtoto wako. Je tunajenga kizazi cha namna gani? Hili ni swali kwa wote ndugu zangu.............................................................. nalia sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Asante

Comment by Dennis Lorishu Paulo on February 20, 2013 at 11:50

Tukubali tukatae mitaala ya elimu ndio mbovu maana kila waziri wa elimu anayeingia analeta lake jipya hadi walimu wanachanganyikiwa wafundishe nini na wanafunzi wanashindwa wasome nini. Iwekwe mitaala inyoeleweka. Pia walimu serikali yetu haiwathamini ndio matunda haya tuliopata ya watoto kufeli. Serikali ikae upya na walimu wamalize madai ya walimu na waombe msamaha kwa walimu kwa maneno waliowatamukia walimu kipindi cha migomo ya walimu.

 

Comment by Tulonge on February 20, 2013 at 10:04

-Pa1 na mengineyo, pia hizi shule zao za kata wanazozianzisha kama njugu bila kupeleka walimu wa kutosha na vitendea kazi zimeongeza hiyo miziro.

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 20, 2013 at 9:59

viongozi wa serikali hawasomeshi watoto wao kwenye hizi shule hohehahe humu ni sisi watanzania wa kawaida ambao hata hatuhitaji mtaala kwa hiyo acheni watukane,wachole,waandike mashahiri ya bongo fleva na kujadili yasio husiana ki taalamu inaitwa extra curriculum kwa tafsiri isiyo rasmi mtaala wa ziada tena kwa maoni yangu wanatakiwa kusahishiwa ni wabunifu.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.....!

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*