Tulonge

Siku moja tu baada ya chuo kikuu cha dar-es- salaam kuwafukuza wanafunzi wake 43,Uongozi wa chuo kikuu cha Afya na sayansi shirikishi muhimbili[muhas], umewasimamisha masomo wanafunziwake 66 kwa tuhuma  za kuwa vinara wa vurugu chuoni hapo.Mbali na hatua hiyo uongozi wa chuo hicho umeeleza  kuwa mipango ya vitisho na uvunjifu wa amani chuoni hapo bado ipo na inaleta hofu kwa walimu na wanafunzi wengine wanaoendelea na masomo.

Makamu mkuu wa chuo Pr. kisali pallangyo, alisema jana kuwa wanafunzi waliosimamishwa  ni wale waliohusika ktk vurugu zilizotokea chuoni hapo december 8 mwaka huu  wakati wa sherehe ya utafiti,na december 10 wakati wa mahafali na jumatatu wiki hii.

Kati ya wanafunzi hao ambao ni wa mwaka wa tatu na tano,kuna msicha.na mmoja tu aliyekumbwa na adhabu hiyo,pr kisali aliongeza uongozi wa chuo una ushahidi wa mkanda wa video na taarifa zingine kutoka vyombo vya usalama.Tatizo la vurugu chuoni hapo ni kuvunjwa kwa jumuiya ya wanafunzi chuoni hapo.

Views: 524

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by cecilia kayombo on December 17, 2011 at 17:29

soooo sad....nchi inazidi kudidimia.

Comment by Silas A. Ntiyamila on December 16, 2011 at 22:13

Nchi hii inanifurahisha, watoto wa wakulima wanalala njaa vyuoni. Bumu hakuna na likiwepo la kupima kwa kijiko lakini cha kushangaza nikuwa wakuwatetea wako mbele kujitetea ili waweze kuchuma mishahara mitatu ya mtu wa kawaida ndani ya siku moja kama posho na bado mshahara wake ambao ni mara 150 ya mshahara wa huyo mlala hoi uko palepale. WAKIGOMA ETI HAWANA ADABU HUKU WAO WALISOMA BURE NA MIKATE WAKIFUNGASHIWA PAMOJA NA USAFIRI WA BURE. Sikatai lakini inauma sana. Ebu waihurumie nchi hii na wanyonge waache kuwanyonga.

Comment by Alfan Mlali on December 16, 2011 at 16:54

Mbona hawatimuani huko bungeni??

Comment by Mama Malaika on December 16, 2011 at 16:23

Nawaonea huruma sana. Yaani mtu unaposomea nyumbani hadi umalize chuo na kufaulu course yako basi wewe uko ngangari kweli kwani kila wakati ni misukosuko tu.

Comment by Tulonge on December 16, 2011 at 16:15

Hawa wanaa mpango wa kufanya nchi iwe na wasomi wachache sasa. Ingekuwa wanawatimua na mafisadi kama hv, ingekuwa bomba sana

Comment by Vitus on December 16, 2011 at 16:06

Kwa mtindo huu vyuo vitabaki na ma-lecturer tu.Wanafunzi hawatakuwepo

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*