Tulonge

MwanaFA "Mfumo wa Analogia urudishwe"

Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ambaye March 13 mwaka huu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa, ameiomba serikali kuwafikiria mara mbili mbili wasanii na kuachia mifumo yote miwili ya digitali na analojia kwakuwa mfumo wa digitali unawaumiza.

Akiongea na gazeti la Habari Leo, FA amesema kwa sasa wasanii nchini wanaumizwa na mfumo wa digitali kwakuwa wamekuwa wakitumia fedha nyingi katika kutengeneza video, lakini zinaishia kutazamwa na watu wachache tu wenye ving’amuzi.

“Waachie mifumo yote kwani kila mtu atakuwa na uamuzi wa kufanya, kutokana na ubora wa kazi,” alisema Mwana FA.

Alisisitiza kuwa huenda akasubiri hata miezi miwili na zaidi, kama serikali itakubali kuachia mifumo yote miwili wa digitali na analojia, na kama hawatotaka, basi ataachia hivyo hivyo kwa kuwa hawezi kukaa nayo ndani.

Views: 199

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on March 20, 2013 at 14:06

Bongo hakufai kabisa maana sirikali inafanya maamuzi ya kidictator. Nchi za magharibi ingawa tuna digital TV bado kuna sehemu watu tunaachiwa option ya analogue.

Comment by Tulonge on March 16, 2013 at 22:48

Kwa hali ya digitali ilivyo mbaya kwa sasa, nakuunga mkono MwanaFA

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*