Tulonge

Mkuu wa Majeshi ya ulinzi,Jenerali Davis Mwamnyange

Mashirika. Mpiganaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ Khatibu Mshindo aliuawa kwa kupigwa bomu juzi na waasi wa M23 kwenye Mji wa Goma ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano makali.

Wakati Mshindo ambaye alikuwa miongoni mwa askari wa Tanzania wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa.

Askari wa Tanzania na wale wa Afrika Kusini wako DRC kwa kazi ya kulinda amani. Malawi bado haijapeleka majeshi yake.

Meja Mshindo alikuwemo katika kikosi cha vifaru na alikuwa kwenye Kambi ya 83KJ iliyoko Kiluvya Dar es Salaam.

Kuuawa kwa askari huyo kumekuja ikiwa ni siku 47 tangu kuuawa kwa askari saba wa Tanzania waliokuwa wakilinda amani kwenye Mji wa Darfur Sudan na Kikundi cha Janjaweed.

Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba alikiri kutokea kifo hicho na kusema: “Jana (juzi) Agosti 28, Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha majeruhi.

“Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.”

Habari zaidi kutoka Congo zinaeleza kuwa mwili wa marehemu Meja Mshindo ulisafirishwa jana kupelekwa Entebbe, Uganda ambako ungefanyiwa matayarisho ya mwisho na tayari kwa kuletwa nyumbani.

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 1129

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Samson Nyansiri on August 30, 2013 at 19:28
Polen sanz
Comment by jemadari mimi on August 30, 2013 at 10:05

poleni sana familia ya mshindo,mkuu wa jeshi la JWTZ mh, davis mwamunyange pamoja na wakuu wa vikosi vingine wa majeshi ,sote watanzania tumeudhunika na kusikitishwa na tukio hilo

Comment by Mjata Daffa on August 30, 2013 at 9:20

Innalilah wainnailayhi rajiun, poleni sana familia ya Mshindo, binafsi nimeumia kwa sababu mshindo ni depo met wangu nimesomanae kuanzia RTS Kunduchi KURUTA hadi munduli.

Tusihuzunike sana ndio ahadi yake, bwana ametoa bwana ametwaa, MUNGU ailaze roho yake pema peponi AMEEN.

Comment by Yusha on August 30, 2013 at 8:11
Poleni sana tanzania

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*