Mkazi wa Magomeni, Yusuf Aboubakar aliyejitolea kufanya kazi ya uokoaji katika jengo lililoporomoka la ghorofa 16 Mtaa wa Indira Gandhi akiwa amepumzika baada ya zoezi la kuondoa kifusi na uokoji kumalizika, juzi. Picha na Fidelis Felix.
Dar es Salaam. Siku ya nne baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka, Yusuf Aboubakar ambaye ni mwokoaji wa kujitolea aliyeopoa miili yote 36, amesema alikuwa tayari kufa kwa ajili ya taifa lake.
Akizungumza jana, Aboubakar (26) alisema hotuba ya Rais Jakay Kikwete ilimgusa na alipata hamasa ya kusaidia watu waliokuwa wamenaswa ndani ya kifusi.
“Nilifika eneo la tukio saa 3:30 asubuhi baada ya kupata taarifa za maafa hayo katika vyombo vya habari. Nikakimbia mara moja kuja kusaidia,” alisema Aboubakar.
Kijana huyu, ambaye hajawahi kusoma shule ya msingi au sekondari ingawa alipata mafunzo kidogo ya uokoaji.
Alisema alipofika eneo la tukio aliomba kuendesha kijiko kilichokuwa kunatumika kwa uokoaji, lakini raia na baadhi ya wanajeshi walimcheka, hakujali.
Alisema aliporuhusiwa alianza kazi na ilipofika saa 8:00 mchana alikuwa wa kwanza kuibua mwili wa kwanza ambao ulikuwa wa mwanamke.
“Ukiniuliza… hata cheti cha darasa la saba sina. Lakini ninajua vitu vingi,” alisema Aboubakar.
Uwezo wa kipekee
Shafii Khalifa, ambaye ni mtu mwingine aliyejitolea kuokoa, alikiri Aboukabar kuwa na kipaji cha ziada cha uokoaji tofauti na wengine.
“Alikuwa anaelekeza tu, ukienda hapo kweli unakuta mwili,” alisema Khalifa.
Khalifa alisema waokoaji wengine walimdharau wakidhani labda ni mwendawazimu, lakini baadaye alikuwa msaada mkubwa katika zoezi zima.
“Hajalala tangu Ijumaa, amekuwa hapa hadi leo (jana) tulipomaliza uokoaji,” alisema.
Aboubakar alisema mwili wa mwanamke huyo ambaye ni mama lishe aliyekuwa akifanya shughuli zake mbele ya jengo hilo, ulikuwa umepasuka tumbo na utumbo wote ulikuwa nje.
Aliendelea kusimulia, ilipofika saa 1:00 usiku aliweza kuopoa miili mingine mitatu na usiku wa manane, miili mingine miwili ilipatikana.
Usiku wa kuamkia jana, miili mingine minne iliyoopolewa na Aboubakar kutoka eneo la varanda ya jengo hilo.
Namna ya kugundua maiti
Aboubakar, mkazi wa Magomeni Kagera, amekuwapo eneo hilo tangu Ijumaa saa 3:30 usiku hadi jana saa 4:00 mchana wakati zoezi linamalizika. Alihusika moja kwa moja na kuopoa miili yote 36 iliyokuwa imefukiwa na kifusi.
“Nina uwezo wa kunusa harufu katika kifusi na kujua kama kuna mwili au la. Cha muhimu ni kumwagia maji juu ya kifusi na unaipata harufu,” alielezea kipaji hicho.
Alisema ili kujua iwapo kuna maiti katika mchanga, unamwagia maji juu ya kifusi, kisha unaifuata harufu ya vumbi inapoelekea na utajua iwapo eneo hilo lina mwili au la.
Aboubakar alisema aliwahi pia kusaidia kuopoa miili ajali ya meli ya Mv Skagit, visiwani Zanzibar.
Alisema katika maiti zote 36, wanawake walikuwa watatu, mamalishe wawili na mwanamke mmoja ambaye anaonekana alikuwa mpitanjia.
Aboubakar ambaye licha ya kutopata elimu yoyote, ana uwezo wa kuzungumza Kiingereza na Kiarabu kwa ufasaha.
Mkandarasi wa Kampuni ya Strabag, ambaye alishiriki uokoaji kwa kiasi kikubwa, Petter Modgran alikiri na kumsifu Aboubakar kwa jinsi alivyojituma.
“Nimemuuliza iwapo amewahi kusomea uokoaji, lakini anasema hajawahi,” alisema Modgran.
Alipata mafunzo Uganda
Hata hivyo, Aboubakar alisema aliwahi kupata mafunzo mafupi ya kijeshi Kapiripiri, Uganda jinsi ya kutambua maiti zilizofukiwa kwenye kifusi, juu ya mti au majini.
Kwa nini ameamua kujitolea kuokoa?
Alipoulizwa nini hasa kilichomsukuma kutumia siku nne kwa shughuli za uokoaji, Aboubakar alisema ni kitu anachokipenda katika maisha yake.
“Nipo tayari kufa kwa ajili ya kuokoa watu wa taifa langu,” alisema.
Aboubakar alisema anachofanya katika maisha yake yote ni kusali, kutenda mema na kusaidia watu wenye matatizo.
Chanzo: mwananchi.co.tz
Add a Comment
Siku zote alikuwa eneo la tukio Mungu amlipe huyu kijana. Si ajabu viongozi wakuu wa uokoaji walikuwa wakitoa maelekezo kwa simu wakiwa nyumbani.
Bila shaka kwa kuwa Amiri Jeshi Mkuu ndiye alisimamia zoezi hili kwa karibu sana hakika hatamuacha kijana huyu awe hana ajira tena awe ni mkuu wa kitengo cha uokoaji na atoe mafunzo kwa vijana maana majanga hayatumi ujumbe lini yatakuja. Hongera sana Sheikh Yusuph Abubakar.
Watanzania wa namna hiyo ni wachache sana, Wakifika 10 watu kama hao tungekua mbele sana kimaisha na kimaendeleo; Kijana wa saa afanye kazi bila kulipwa ndoto za Alinacha
Hakika kila mwanadamu ana karama yake, na kila karama hutoka kwa Mwenyezi Mungu!
Malipo ya Yusuf yapo mbinguni! Kwa maana hapa duniani hajapata chochote zaidi ya kumsifu.
Duuh Mama Malaika nimelipenda somo lako kwa kweli
Daaah kweli mungu ana maajabu yake,ina mana mshkaji hata darasa moja hana lkn hodari hata mie sifai
Aboubakari we ni noma tufundishane tuwe wengi ili taaluma isipotee,mimi nimekukubali mungu akupe maisha marefu.
-Nimependa maelezo yako Mama.
-Christer usimalo linaweza kuwa kweli, utashangaa mtu kama huyu anaachwa tu wakati ni mtu muhimu sana kwa Taifa letu. Ingekua poa sana kama angeendelezwa zaidi katika kazi ya uokoaji na hatimaye TZ tuwe na mtaalamu wa kujivunia.
Tumelazimika kuleta wataalam toka nje bila kujua kuwa tunaye mtaalam hapa hapa TZ. Kama asinge jitokeza mwenyewe ingekuaje? Tumesha tambua sasa tunaye mtaalam, TUMTUNZE SASA. Siyo tumsahau.
Mungu akujalie Aboubakar uzidi na moyo huo huo. Hao walio mdharau ndio wajinga wa mwisho.
Wanasayansi (psychologists) wanasema kila binadamu kazaliwa na sixth sense tatizo wengi hatujui na wala hatujitambui kuwa tuna uwezo wetu wa sixth sense kwa kutumia extrasensory perception (ESP) ambazo ni sense of smell, sight, sound, touch & taste. Kwa kuwa dini zinapingana science, hivyo husikii term hii ya sixth sense bali term inayotumika kwenye dini ni Divine Power.
Kuna watoto wadogo wanafanya maajabu kwa kutumia extrasensory perception (ESP) kwani huhitaji kujua kuandika au kusoma ku-develop sixth sense bali ni uwezo wako ku-connect your body and mind kwenye mazingira uliyopo na kutumia 5 elements (water, earth, fire, wind and ether) kujua vitu beyond our imagination, our natural world. Aboubakar katumia smell and water (kumwagia maji kwenye kifusi) ku-sense kama kuna maiti chini ya kifusi. Binadamu wanao weza kutumia sixth sense organs (smell, sound, taste, touch and sight) kwa kuziunganisha na 5 elements (water, air, earth, fire and ether) wanafanya vitu vingi sana ambavyo kwa mtu asiyejua sixth sense ni nini aweza sema ni uchawi kumbe ni uwezo wa binadamu alopewa na Mwenyezi Mungu.
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge