Tulonge

Nassari Akitoa Damu kwa Majeruhi Mlipuko wa Bomu

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari Akitoa Damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi wa mlipuko wa bomu Leo jijini Arusha

wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari Akitoa Damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi wa mlipuko wa bomu Leo jijini Arusha. Nassari Akitoa damu kwa Majeruhi Mlipuko wa Bomu
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari mbali ya kuwahamasisha watu kutoa damu, pia hivi punde amemaliza kutoa damu kwa ajili ya kuwachangia majeruhi waliolipukiwa na bomu kanisani LEO. Pichani Nassari akionekana akitoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari LEO tangu majira ya saa 5:30 asubuhi wamekuwa wakifanya kazi ya kuwahamasisha watu kutoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi mbalimbali waliojeruhiwa na bomu katika kanisa la Parokia Mpya ya Olasiti mjini humo.

Kutokana watu wengi kupoteza damu na kumwagika kwa wingi. Mbali na hilo baadhi ya wahudumu wa hospitali hiyo wameueleza mtandao wa Habarimasai.com kwamba hivi sasa wana wakati mgumu katika kufanya usafi na mwandishi wetu Joseph Pantaleo ameshuhudia manesi hao wakisafisha damu sakafuni kila wakati huku wakimwaga maji na dawa ili kuondoa mabaki ya damu hiyo.

Lema na Nassari wameonekana wakiwahamisisha watu kutoa damu na wengi wameitikia wito huo.

Chanzo: habarimasai.com

Views: 431

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on May 6, 2013 at 12:46

Hongereni wanamapinduzi wazalendo maana wanasemaga mnahamasisha vurugu tu, yuko wapi MAGESA MULONGO. Tusaidiane kuwaondoa hawa wakoloni wa kiafrika madarakani.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*