Tulonge

Nauli ni Kiama: Sumatra yapandisha nauli za daladala, mabasi ya mikoani, treni na meli

Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imepandisha nauli za daladala, mabasi ya kwenda mikoani, usafiri wa reli na tozo za majini kuanzia Aprili 12, mwaka huu.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Ahmad Kilima alisema jana kuwa nauli za daladala zimeongezeka kwa asilimia 24.46 kwa kuzingatia maoni ya wadau na gharama za uendeshaji.


Kwa upande wa usafiri wa daladala nauli zimepanda kwa umbali tofauti kutoka Sh300 hadi 400, Sh350 hadi 450, Sh500 hadi 600, Sh650 – 750 na kwa wanafunzi kutoka Sh150 hadi 200 katika sehemu yoyote watakayokwenda.


Nauli za usafiri wa mabasi makubwa ya masafa marefu nauli hizo zimeongezeka kwa viwango tofauti. Mathalan kwa basi la kawaida kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya ni Sh30,700, njia ya vumbi kutoka Kigoma hadi Sumbawanga Sh25,400 na basi la hadhi ya kati (Semi Luxury) kati ya Dar na Mwanza ni Sh61,400, wakati basi la hadhi ya juu (Luxury) kati ya Dar na Arusha ni Sh 36,000.


Kilima alisema: “Kuanzia Aprili 12 mwaka huu, kati ya kilometa 0 hadi 10, nauli ya daladala itakuwa Sh400 badala ya Sh300 zinazolipwa hivi sasa.
“Pia nauli za mabasi ya kwenda mikoani zimeongezeka kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida, mabasi ya kati kwa asilimia 16.9 na mabasi ya daraja la juu kwa asilimia 13.2,” alisema.


Kilima alisema nauli za mabasi ya mikoani zimepanda kutoka Sh30.67 hadi Sh36.89 kwa kilometa kwa mabasi ya daraja la kawaida katika njia za lami.
Kwa upande wa mabasi ya kawaida kwa njia ya vumbi imepanda kutoka Sh37.72 hadi Sh 46.11 kwa kilometa na kwamba mabasi ya hadhi ya kati, nauli zimepanda kutoka Sh45.53 hadi Sh 53.22 kwa kilometa.


Alisema mabasi ya hadhi ya juu nauli zimepanda kutoka Sh51.64 hadi Sh58.47 kwa kilometa.
“Kupanda kwa nauli kunatakiwa kwenda sambamba na huduma bora na kwamba Sumatra imepiga marufuku kutumia wapigadebe kuuza tiketi za safari”alisema.

Usafiri wa Reli
Katika uamuzi huo, usafiri wa reli pia umepanda ambapo daraja la kwanza Dar es Salaam hadi Morogoro, nauli mpya na ya zamani katika mabano ni Sh21,100, (Sh16,852), Dar hadi Dodoma Sh34,700, (Sh27,788), Dar es Salaam-Tabora Sh54,800, (Sh43,859).
Dar es Salaam-Isaka Sh62,100, (Sh49,662), Dar- Shinyanga Sh65,300 (Sh52,229) Dar –Mwanza Sh74,800 (Sh 59,818), Dar- Kigoma Sh75,700, (Sh60,599)


Daraja la pili, Dar es Salaam-Morogoro Sh16,600, (Sh13,280), Dar es Salaam-Dodoma Sh26,400 (Sh 21,092), Dar es Salaam-Tabora Sh40,500 (Sh 32,364), Dar es Salaam-Isaka Sh45,800, (Sh36,605), Dar es Salaam-Shinyanga Sh48,000 (Sh38,390), Dar es Salaam- Mwanza Sh54,700 (Sh43,747), Dar es Salaam-Kigoma Sh55,400 (Sh44,305).


Daraja la tatu, dar es Salaam-Morogoro Sh8,800 (Sh6,138), Dar es Salaam-Dodoma Sh13,500 (Sh9,374), Dar es Salaam-Tabora 20,400 (Sh14,173), Dar es Salaam-Isaka Sh22,800 (Sh15,847), Dar es Salaam –Shinyanga Sh24,000 (Sh16,628), Dar es Salaam-Mwanza Sh27,200 (Sh18,860), Dar es Salaam- Kigoma Sh27,500 (Sh19,084).


Akizungumzia tozo za majini, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mamlaka hiyo imeridhia ongezeko la tozo la asilimia 34.3 kwa vyombo vinavyotumia bandari za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).


Alisema awali TPA walipendekeza tozo hizo kuongezeka kati ya asilimia saba hadi 400 kulingana na aina ya huduma zinazotolewa kwa meli zinazotumia bandari za mamlaka hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz

Views: 521

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on April 3, 2013 at 20:04

Gharama za maisha tu ndo zinazidi kupanda lakini,lakini kipato na mishahara ndio utashangaa

Comment by Jeath Justin Prosper on April 3, 2013 at 14:49

Nadhani kuna wakati elimu inakuwa haina maana kuwa nayo.sijaona vigezo vya msing kwa kupandisha nauli......kwa nini wazungumzie kupanada kwa gharama ya uendshaji?nani ana control ghrama kama si serikali. ni maajabu sana kwa TZ mafuta yako juu kiliko "land locked countries" na wakati mafuta hayo hupitia bandari ya Dar es salaam. 

Cha msingi serikali kwa kuwa wamezidiwa, wapandishe nauli ya daladala mpaka 1000. Magari yote ya serikali sasimamishwe kufanya kazi kuanzia ST,SU,DFP,JW,PT na zingine....halafu waondoe kodi zote za uingiaji wa magari toka nje ili kila mwananchi amiliki gari yake na hayo ya serikali yageuzwe kuwa school bus. kwa sababu kuna magari yanauzwa japan USD 750. hii kila mwnanchi anaweza kuingiza nchini na asipande tena hyo madaladala. ila gari hiyo ikiletwa unakuta mtu mpaka alimiliki analipa zaidi ya dola za kimarekani 3000.

Comment by Mama Malaika on April 3, 2013 at 14:36

Hivi Tanzania haina institution inayoitwa Bunge la Jamhuri kupitisha mapendekezo ya nauli kama wafanyavyo nchi zilizoendelea??? Kutokana na mshahara wa kawaida wa mtanzania hiyo nauli ni kubwa sana, au kwa kuwa wa TZ wanakuwa ukimya basi kila Mamlaka zinajichukulia sheria mkononi??? Hiyo si democracy bali ni dictatorship.  

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*