Tulonge

Ni rahisi kupata taarifa za timu za Ulaya kuliko za Kiafrika

Teknolojia imekuwa sana siku hizi, kuwasiliana siyo lazima simu, barua au faksi kama ilivyokuwa zamani. Njia kama baruapepe na simu za mkononi ni haraka na zenye ufanisi mkubwa katika mawasiliano.

Tofauti kati ya taasisi za michezo na taasisi nyingine ni kuwa hizi za michezo zina mashabiki ambao lazima wapewe taarifa kila inapobidi. Kabla ya kuanza kwa msimu wa 2010/2011, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilizitaka klabu zote za Ligi Kuu kuajiri ofisa habari ambaye atakuwa na kazi ya kutoa taarifa rasmi kwa mujibu wa timu husika.

Shirikisho lenyewe lilikuwa la kwanza kuwa na ofisa habari, wakati huo akiwa Florian Kaijage nafasi ambayo sasa inashikiliwa na Boniface Wambura.

Katika kipindi cha kuwa na maofisa habari, tumeshuhudia mabadiliko kidogo katika klabu, likiwamo suala la utoaji habari.

Pamoja na msisitizo kutoka TFF, bado ni klabu chache sana ambazo zimeweza kutumia fursa hii kuwasiliana na wanachama wake. Maofisa habari wengi wamekuwa wakisikika pale tu wanapotafutwa na vyombo vya habari, wengine hata mashabiki wao hawafahamu majina yao.

Ulimwengu wa sasa unategemea mawasiliano ya mtandao zaidi katika kuwasiliana. Ajabu kuwa timu zetu na hata shirikisho hawaweki uzito katika utoaji wa habari kwa njia ya mitandao.

Licha ya kuwa na maofisa habari, timu za Ligi Kuu hazina mfumo mzuri wa utoaji habari kwa njia ya mtandao.

Miezi kadhaa nyuma, tovuti ya TFF ilifungwa na wasimamizi wa seva, jambo ambalo pengine lilisababishwa na kutokulipia huduma za kuhudumia tovuti kwa kipindi fulani, aibu hii haikuwekwa sana hadharani. Tovuti ya klabu ya Simba, http://www.simba.co.tz/ nayo ina matatizo hayohayo ya kufungwa na hakuna mwanachama aliyeonekana kuguswa na hili.

Mtibwa Sugar ilikuwa ndiyo timu ya kwanza kuwa na tovuti hai mwaka 2007, lakini kati ya timu zote, Yanga na Azam ndiyo zenye huduma hai za tovuti, kwa maana unaweza kupata habari za karibuni katika tovuti zao.

Katika pitapita zangu mtandaoni, nilikuta tovuti ya Coastal Union ikiwa na habari za kutua kwa kiungo kutoka Brazil, Gabriel Barbosa kama habari mpya. Taarifa ambayo ina zaidi ya miezi sita tangu itolewe.

Huu siyo ulimwengu ule wa kusubiri saa 1:40 jioni ifike ili usikie jinsi mwenyekiti wa Chama cha Soka anavyotupiana matusi na mtangazaji wa kipindi cha redio. Ni wakati ambao mtu anaweza kupata taarifa wakati wowote na mahali popote.

Wakati nchi zilizoendelea zikitumia fursa hii kuwasiliana na mashabiki wao, Tanzania bado tunasubiri mkutano mkuu mara moja kwa mwaka ili kufikisha dukuduku letu kwa uongozi.

Ni rahisi kupata taarifa za timu za Ulaya kuliko timu zetu za Kiafrika, kwa kuwa klabu bado hazijaona umuhimu wa kuwa na idara za habari zenye ufanisi na siyo tu kuishia kuwa na ofisa habari mmoja.

Mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter ni nyenzo nyingine ya utoaji habari ambayo klabu na mashirikisho yetu ya michezo imepuuza. Homa ya mawasiliano haiishii kwa TFF na wanawe pekee, hata katika vyama vingine nako hali ni moja. Vyama vingi havina tovuti wala kurasa za mitandao ya kijamii.

Mapinduzi ya kiufundi katika michezo nchini yanatakiwa, kuambatana na mapinduzi ya kiutawala. Habari ni kiungo muhimu kati ya taasisi na wadau wake, nafasi yoyote itakayopatikana ya kuboresha hali ya habari itumike ipasavyo.

Mphamvu Daniel ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 0717 474 832.

Via: mwananchi.co.tz

Views: 125

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*