Tulonge

"Nitaanika kila kitu baada ya siku 40 kuanzia sasa" - Dkt. Ulimboka

Na Gabriel Mushi, Gabriel Masese via gazeti la MTANZANIA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Stephen Ulimboka, amesema anatarajia kuanika madudu ya watu waliomteka na kumfanyia vitendo vya kinyama, baada ya kufanya uchambuzi wa kina mkasa uliomkumba.

Akizungumza katika mahojiano maalum na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Dkt. Ulimboka alisema ataanika madudu yote aliyofanyiwa, baada ya siku 40.

Dkt. Ulimboka, aliyerejea kutoka nchini Afrika Kusini, alikokuwa amekwenda kutibiwa, alisema ana siri nzito moyoni ambayo akiitoa, Watanzania watamuelewa tu.

Alisema baada ya kurudi nyumbani salama, hivi sasa amejikita zaidi kufanya uchambuzi wa mambo au matukio yaliyomsibu kabla ya kupelekwa Afrika Kusini ili ukweli ujulikane.

“Nawaomba Watanzania wawe na subira kwanza, nitaanika kila kitu baada ya siku 40 kuanzia sasa, jambo kubwa ninaloangalia sasa ni kuimarisha kwanza afya yangu ambayo Mungu amenipigania vya kutosha, baada ya hapo nitaeleza kwa kina mkasa huu ulionikuta wakati wa mapambano ambayo nyote mnayajua. Napenda kuwahakikishia Watanzania na madaktari wenzangu, kuwa nitaendelea kusimamia kile ninachoamini na kukitetea…nitaendelea kuongoza Jumuiya ya madaktari, nitaendelea kujiamini ili kuhakikisha tunapigania madai yetu,” alisema Dkt. Ulimboka.

Kuhusu familia yake, kama inaweza kutoa tamko, Dkt. Ulimboka alisema hafahamu iwapo familia imeandaa mpango huo, lakini kwa upande wake, wakati ukifika atalitoa mbele ya umma kama ilivyo kawaida yake kwa ushahidi wa kutosha, “Kuhusu suala la uchunguzi, siwezi kulizungumzia sana kwa sababu kama nilivyosema siwezi kukurupuka kuanza kutoa ushirikiano na Jeshi la Polisi, wakati sijausoma mkasa wenyewe kama unaendelea vipi. Nimesikia baadhi ya vyombo vya habari, vikisema nimefichwa, jamani sijafichwa na familia…. naendelea na shughuli zangu kama kawaida, lakini jambo la msingi ni kuimarisha kwanza afya yangu, kabla ya kuanza kukutana na waandishi wa habari hadharani,” alisema Dkt. Ulimboka na kuongeza, “Nipo kwenye mihangaiko yangu na muda huu nipo safarini, naelekea mjini Bagamoyo.”

Katika hatua ya kushangaza, Dkt. Ulimboka aliamua kutumia usafiri wa boti kwenda Bagamoyo, tofauti na siku ambazo amekuwa akitumia njia ya barabara.

Hii ni mara ya kwanza Dk. Ulimboka kuzungumza kwa kina na MTANZANIA, tangu aliporejea kutoka nchini Afrika Kusini, ambako alikwenda kutibiwa Juni 27, mwaka huu.

Wakati Dkt. Ulimboka akisema hayo, ofisa mmoja wa Jeshi la Polisi nchini, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, aliiambia MTANZANIA kuwa, hivi sasa jeshi hilo linaendelea na vikao ili kuona ni namna gani wanaweza kushughulikia suala la Dkt. Ulimboka.

Habari za kuaminika kutoka kwa ofisa huyo, ni kwamba Ijumaa wiki hii linaweza kutoa ufafanuzi zaidi au hatua zitakazochukuliwa dhidi ya daktari huyo.

Views: 654

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by manka on August 16, 2012 at 13:10

hee mbona mi sielewi sasa wanachukua hatua zidi yake kwani yeye kafanyaje? DK. fanya fasta waumbue kabla na wewe hatujaambiwa umefia ughaibuni ukachomwa moto.

Comment by ILYA on August 16, 2012 at 0:17

Nilitegemea kusikia Jeshi la Polisi likimpa ushirikiano wa karibu mheshimiwa Dr.Ulimboka na kuwatia hatiani wale wote walioshiriki kumkabidhi maumivu hayo aliyopata kionevu! lakini ni ajabu habar hii inasema kwamba: Ijumaa wiki hii linaweza kutinga na ufafanuzi zaidi kunako hatua zitakazochukuliwa DHIDI ya Dakta ULIMBOKA!!.Ni ajabu sana,anatoka katika mitikasi ya kutibiwa ili kurudisha afya yake,kafanyiwa uovu na unyankuzi na watu hao waovu,lakini jeshi l polisi liko kimya,halijatoka kwend kuwasaka waliomtendea unyama,hawajafanya kila walilotakiwa kulifanya,lakini wanaahidi kuchukua hatua dhidi ya Ulimboka aliyepata dharba kinyume na sheria kutoka kwa wahuni hao.!! sielewi ni which kind of government we have?!

Comment by ANGELA JULIUS on August 15, 2012 at 15:28

BADO NAKIMBIA TENA DUKANI KUNUNUA SENENE NA ILE POMBE YA KWETU HUKU NIKISUBILI HABARI KAMILI ZENYE UKWELI AMABAZO NILIKUWA NIKISUBILIA MUDA MREFU, MIMI BINAFSI NAKUTAKIA KILA LA KHERI DK NA UONGEEEEE YOTEEEEE NA PIA NAIOMBEA NCHI HII TUFANYE MABADILIKO YA 2015 TUWEKE CHAMA TOFAUTI NA HIKI CHA KIJANI KIBICHI ILI HAKI ITENDEKE VIZURI MANAKE WATAENDA WENGI JELA. MUNGU IBARIKI TANZANIA

Comment by York David Drexell on August 15, 2012 at 15:27

WHY 40 DAYS?

WATU HAWAKUSUBIRI SIKU 40 KUFA WAKATI MADAKTARI WAKIWA KATIKA MGOMO!!!!.

Comment by EMMANUEL ALBERT FUNGO on August 15, 2012 at 14:44

Tuna amini sasa ni saa ya Mungu kuanika ukweli na Mungu akusaidie kuafanya uchambuzi wa kina na yakinifu ili wasikutege kwa jingine tena kuwa na msimamo ndo jambo la msingi sana

 

Comment by Tulonge on August 15, 2012 at 12:32

Kaka hizo siku 40 mbona kama nyingi sana, wasije wakakubananisha tena. Sasa hv akikukamata watakusagasaga uwe kama umekanyagwa n treni.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*