Tulonge

Njaa inatesa watoto jamani, kuna mdau yoyote anayefahamu nini kiliendelea atufahamishe

Katika pitapita zangu nimekutana na hii picha sehemu ila haikuwa na maelezo ya kina. Picha inaonesha mtoto akiwa hali mbaya inayosemekana ilisababishwa na kukosa chakula, pembeni yake kuna ndege mkubwa ambaye anasubiri mtoto afariki ili aweze kumla.

Kila mtu anasema lake, kuna baadhi wanasema kuwa huyo mtoto wa kike alifariki na baadae kuliwa na huyo ndege. Wapo wanaosema kuwa mpiga picha zalimfukuza ndege na kuondoka na huyo mtoto ingawa baadae alifariki kwa njaa maana alikuwa katika hali mbaya sana.

Sijapata uhakika nini kiliendelea hapo, kama unafahamu lolote unaweza kutufahamisha.

Njaa ni moja kati ya majanga yanasotikisa nchi nyingi Duniani kwa sasa.Inabidi ushukuru Mungu sana endapo unapata ridhiki ya kuitosheleza familia yako kwa siku.

Views: 661

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by jemadari mimi on January 12, 2012 at 15:36

Hivi unampa zawadi ya mwandishi bora muuaji huyu mzungu,mshenzi kabisa amedhalilisha taaluma ya habari,tena hafadhli alivyokufa

Comment by jemadari mimi on January 12, 2012 at 15:22

Hakika binadamu ni kiumbe dhaifu kuliko kiumbe chochote hapa duniani,ebu muangalie huyu mtoto hajui atapata wapi matumaini ya kuona raha ya maisha ,hapa ndipo walipotufikisha viongozi wa bara hili  la afrika wanajijali sana wao kuliko raia zao,maskini kijana wa watu alikufa kwasababu ya njaa tu,siwezi kulaumu wazazi wake kwanini wamemzaa ila nalaumu serikali yake kwa kutofanya jitihada ya makusudi kuokoa maisha yake.

lkn bonn inawezekana ni kweli ni jamii ya wafugaji hawa,ila waliitaji msada wa serikali juu ya kuwapa chakula na ikiwezekana kupewa ushauri juu ya athari za kutokulima na kuhifadhi chakula

Comment by Bonielly on January 9, 2012 at 10:24

mmemuona yule ndege pale nyuma ya huyo dogo? halafu hawa ni jamii ya wafugaji huwa hawajihusishagi na kilimo kabisa huwa wanafuga mifugo mingi, mifugo ikishikwa na ugonjwa au njaa na hao huwa wanapata shida sana maana hawajui kulima, mungu nusuru watu hawa wape maarifa,

Comment by Alfan Mlali on January 8, 2012 at 11:56

Nilipata kusikia kuwa huyo mtoto alikuwa akielekea kwenye kambi ya kutoa misaada iliyokuwa umbali wa zaidi ya kilomita 6 kutoka hapo alipopigwa picha. Kutokana na kuzidiwa na njaa akashindwa kutembea akawa anatambaa huku tai akimfuatilia kwa nyuma afe ili amtafune....Sasa hilo lipiga picha la kizungu likaona bora picha na si kumsaidia KUMFIKISHA KWENYE HIYO KAMBI APATE MSAADA..!

Comment by Alfan Mlali on January 8, 2012 at 11:52

Kwa kifupi napenda kusema "Alhamdulillah" kwa alichonijaalia M/Mungu!

Tusiombe njaa itokee jamani..Mungu atuepushie mbali.

Comment by Gratious Kimberly on January 8, 2012 at 4:16

Inasikitisha  naona dada wa kisuma  Pili hapo chini katoa story iliyo makini!!

Comment by Mama Malaika on January 7, 2012 at 23:01

Hii picha ina story ndefu sana. UK (Channel 4) miaka ya nyuma nimesahau nafikiri ilikuwa 2004 au 2005 waliwahi onyesha documentary kuhusu hii picha na kumuelezea mpiga picha wa hii picha aliyeitwa Kevin Carter. Na mwisho wa hiyo documentary inaishia kusema kwamba kuwa Kevin Carter na hata rafiki wa Kevin Carter aliyeambatana naye huko Sudan kusini hakujua nini hatima ya huyo mtoto.

Kama una roho ndogo ukiona hiyo documentary unalia machozi kwani Kevin Carter alipiga picha nyingi sana huko Sudan kusini za watoto wenye njaa wengine wanakata roho.

Comment by Tulonge on January 7, 2012 at 22:34

Comment by Tulonge on January 7, 2012 at 22:29

Comment by manka on January 7, 2012 at 19:36

EE Mwenyeenzi Mungu nakushukuru kwa chakula unachonijalia, mwangalie kiumbe huyu aliye mbele yako akiwa amekosa tumaini la kuishi kutokana na njaa kali inayomsibu, urudishe tena tumaini kwake kwa kuwa wewe ni mwema na unawaangazia wema wako walio wema na wabaya.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*