Tulonge

Nkasi: Wafanya upasuaji kwa kutumia tochi

LICHA ya Kituo cha Afya cha Kirando mwambao wa Ziwa Tanganyika Wilayani Nkasi kuwa kituo pekee cha tiba mkoani hapa, kinachofanya upasuaji na kutoa damu salama, hakina umeme hali inayosababisha wauguzi kufanya upasuaji kwa kutumia mwanga wa simu zenye tochi.

Hayo yalibainishwa jana na Mratibu wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama Tanzania, Rose Mlay katika mkutano wa siku moja uliwajumuisha viongozi wa dini, viongozi wa asasi za kijamii, wataalamu wa afya na uongozi wa mkoa wa Rukwa uliofanyika mjini hapa Kwa mujibu wake kituo hicho cha afya kinakabiliwa pia na ukosefu wa mashine ya hewa safi ambayo ni muhimu wakati wa upasuaji na kumsaidia mtoto mchanga mwenye matatizo ya kupumua.

Pia kina wataalamu wachache.

“Ili akina mama wapate huduma za dharura za uzazi karibu nao Serikali iliahidi Kituo cha Afya kijengwe katika kila kata na asilimia 50 ya vituo hivyo kutoa huduma za uzazi za dharura kama upasuaji kumtoa mtoto aliyekwama na kutoa damu salama,” alisema.

Aliendelea kusema, “maendeleo yapo kwa mfano mkoani hapa kuna vituo vya tiba 10 vya Serikali na viwili vinavyomilikiwa na madhehebu ya dini, lakini kwa bahati mbaya sana hakuna hata kituo kimoja kinachotoa huduma kamili za uzazi za dharura".

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk Emanuel Mtika alisema licha ya vifo vya wajawazito kupungua hadi kufikia 127 kwa vizazi hai 100,000 bado idadi ya vifo hivyo ni kubwa.

Akitoa mfano, Dk Mtika alisema tangu Januari hadi Septemba mwaka huu, wajawazito 31 wamepoteza maisha wakati wa kujifungua katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa baada ya kucheleweshwa kufikishwa hapo.

“Akina mama hao walifikishwa hospitalini hapo wakiwa katika hali mbaya sana hivyo wote 31 walipoteza maisha kwa vipindi hivyo tofauti, hii ni kutokana kwanza wanapokaribia kujifungua hufikishwa kwanza kwa wakunga wa jadi na kisha wakizidiwa hukimbizwa katika vituo vya tiba vilivyopo karibu nao kabla ya kufikishwa kwetu", alisema.

Chanzo: habarileo

Views: 191

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*