Tulonge

Obama atishia kusitisha uhusiano na Uganda endapo itapinga ushoga

Rais wa Marekani Barrack Obama amemwonya rais wa Uganda,Yoweri Musuveni, kwamba ikiwa atasaini mswada wa sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja basi uhusiano kati ya Uganda na Marekani utatatizika.

Chini ya sheria hiyo iliyopendekezwa, watu watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ushoga watakabiliwa na hukumu kali, ikiwemo kifungo cha maisha jela.

Marekani ni mojawepo wa mataifa ya kigeni yanayotoa kiwango cha juu zaidi cha msaada kwa Uganda, na mwaka 2011 idadi ndogo ya wanajeshi wa Marekani walitumwa kulisaidia jeshi la Uganda kupanda na kundi la waasi wa Lords Resistance Army, LRA.

Lakini Rais Obama amesema uhusiano huo unaodhaminiwa sana utatatizika zaidi iwapo mswada huo wa kupinga mapenzi ya jinsia moja utaidhinishwa na kuwa sheria.

Ameeleza kwamba mswada huo ni wa kidhalimu na hatari kwa jamii ya mashoga nchini Uganda.

Mshauri wa maswala ya usalama nchini Marekani, Susan Rice, amesema kwenye mtandao wa Twitter kwamba amefanya mazungumzo ya kina na rais Museveni jumamosi usiku kumtaka asitie saini mswada huo.

Mbali na Uganda rais Obama amelalamika kwamba visa vya mashambulizi na kuhangaishwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja vimeenea katika mataifa kadhaa kutoka Urusi hadi Nigeria.

BBC Swahili

Views: 1458

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by KUNAMBI Jr on March 17, 2014 at 15:06

kwa hili hata me namuunga mkono Museven,sasa Kikwete atatoa jibu gani?

Comment by Mama Malaika on March 5, 2014 at 19:06
Okay.. CHA. Naomba turudie na roho nyepesi (kind soul), tuko kwenye mwezi mtukufu. Ha ha haaaa....
Pia kumbuka kuwaombea mashoga kwani kwa Mungu hakuna gumu iwapo tunatumia rational approach. Mfano ni hii link ya Tulonge, jamaa alikuwa shoga na kaamua kuuacha ushoga
http://tulonge.com/profiles/blogs/aunt-asu-aamua-kuacha-ushoga-na-k...
Comment by CHA the Optimist on March 4, 2014 at 19:22

Aya! Ngoja niwarudie.

Comment by Mama Malaika on March 4, 2014 at 12:18
Oops... I mean east, na sio west. Nisamehe...
Comment by Mama Malaika on March 2, 2014 at 1:00
Karibu Chaoga. June 03 calendar ya kanisa Catholic ni siku yao. Wa-Ganda wengi husikii wanakwambia kisa cha ushoga ni mojawapo ya sababu za mauaji ya Mashahidi wa Uganda au Kabaka Mwanga II alikuwa shoga, wanaona aibu. Wa-Ganda wachache sana wanasema kisa hicho. Mie naomba Mungu kusiwepo na mtu wa hali hiyo kwenye ukoo wetu.

Tena Chaoga katika safari zako za Uganda siku moja fika Namugongo. Ukiwa Kampala City centre elekea west of the city na ukamate Jinja road (A109) na kwa mbele kushoto ndio Namugongo iko hapo kanisa kubwa, na wamezikwa Mashahidi (si wote). Ni dakika kama 50 hivi (driving). Au pale city centre wamwambia taxi driver akupeleke Uganda Martyrs Shrine, atakufikisha bila shida, ni sehemu maarafu sana
Comment by chaoga on March 1, 2014 at 17:45

ahsante mama kwa kuniongezea maarifa, historia ni muhimu kuijua kabla hujajenga hoja

Comment by Mama Malaika on March 1, 2014 at 17:38
Nadhani baadhi mlishasikia "Mashahidi wa Uganda" (watakatifu wa kanisa). Inaonyesha kuwa vutendo vya ushoga vilikuwa kawaida kwenye ufalme wa Baganda kabla ya wageni kuingia Uganda 1870s. Baada ya wageni kuingia na wenyeji wakaanza kushika dini hivyo King Mwanga (Kabaka Mwanga) na wenzie alichukizwa na vijana wa kiume ambao walikuwa wame convert to Christianity kumkatalia kushiriki vitendo vya ngono (ushoga) na akaanza kuwaua mwaka 1885 hadi 1887. Na siku ya tarehe 3 June mwaka 1886 peke yake aliwachoma moto waumini 40 na kitu ambao ni wakatoriki na wa Anglican. Na hiyo ni miaka 130 imepita kitu ambacho kinaonyesha baadhi ya waganda walikuwa na tamaduni ya ushoga kwenye jamii yao kabla ya wageni kuingia.

Uganda kuna sehemu yaitwa Namugongo ambako kuna Namugongo Minor Basilica ipo miaka mingi sana, hapo pamejengwa shrine miaka ya 1960s kuwakumbuka Mashahidi wa Uganda. Na hapo utasoma history (ukweli) wa mauaji hayo, na baadhi ya vijana walio nusurika na mauaji yale walililewa hapo hadi walipokuwa vikongwe na kufariki. Na hapa Westminster Abbey (kanisa London), kwenye lango kuu la kuingilia kwa juu kumewekwa sanamu kuwakumbuka Mashahidi wa Uganda, na wana siku yao husomewa Misa mara moja kwa mwaka
Comment by Mama Malaika on February 28, 2014 at 21:39
Ha haa haaa.... Zainabu. Ujue CHA the Omniscient ni mzee wa kanisa, asije na Bible yake hapa akanipa radhi bure. Ha haaaa....

CHA... Wana siasa wasanii sana. Museveni angekuwa jasiri hivi kwenye natural resources anazoachia marafiki zake wazungu wanabeba kunufaisha nchi za west ningemuona wa maana sana. Hapo ukute miezi si mingi Museveni ataingia White House kupata dinner na Obama. Waswahili wapemba hao wajuana kwa vilemba. Na sheria hii ya ushoga ukute itabana mashoga walalahoi na sio mashoga wale mapapa. Na hivyo ndivyo wanavyofanya waarabu kwao wana sheria kali au ushoga na ulevi lakini watoto toka koo ya kifalme (the Saudi royal family members) wakishikwa na ushoga au ulevi wanaachiwa.
Hawa wana siasa wanajua sana kuchezea akili za watu, siwaamini, hapo ukute wana matatizo yao hivyo wanatumia ushoga as scapegoats (for political means) to distract the population from the government's corruption and disorder. Museveni miaka hii 2 kashutumiwa na wananchi wake kwa corruption, kubana upinzani na watu kupotea (ana waua) mara waandishi kupigwa, n.k. Na bado nchi wafadhili wamemshutumu kwa kuiba/kula pesa wanazotuma za misaada kiasi kwamba baadhi wao (Denmark, Norway, n.k) wametumia hii issue kukata misaada, na watao athirika ni walalahoi wanaotegemea misaada na sio Museveni na wenzio wanaojilipa posho kubwa.
Obama naye kwake US kumechacha hivyo ana zuga zuga kwani kwake wamemkomalia kuhusu masuala ya uchumi. Week hii nimemsikia kwa Museveni na pia juu ya mapinduzi ya Kiev (kumpingeza kiongozi mpya wa Ukraine) na hiyo yote ni kumuuzi Vladimir Putin wa Russia anayejutahidi kuzuia nchi za former Soviet Union kwenda pande ya magharibi (west Europe). Kazi kweli kweli.....
Comment by Zainabu Hamis on February 28, 2014 at 18:52

Omniscient against Mama Malaika. Maana naona mmetofautiana; aya mie na Tulonge ngoja tuwasikilizeni kwanza,ili tupate madesa ya kutumia kwa mjadala huu.

Comment by Mama Malaika on February 28, 2014 at 16:08
Mie nimekuelewa Chaoga. Tatizo sirikali za Africa hazina tamaduni ya kujali Haki za Binadamu.
Hili suala ni mtihani... Mungu muumba na mwenye mamlaka ya kuhukumu viumbe wake ndio anayejua na atahukumu. Dini (mie mkristo) inasema usinyooshe kidole kwa mwenzio au kumuhukumu, jiangalie kwanza mwenyewe kama uko msafi (boriti).

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*