Othman Michuzi
Mdau Msema Kweli anasema:— Mwanalibeneke Othman Michuzi a.k.a “m2 ya mtaa kwa mtaa” wa Michuzi Media Group juzi alitinga ndani ya Kilimanjaro Music Award katika ukumbi wa maraha na burudani pale Mlimani City, jijini Dar.
Alichokifanya Othman kwa kutumia kamera yake au Jicho Kubwa lionalo mbali, ni kurekodi video ya matukio, ambayo video hiyo inawezekana ikawa ndiyo tiketi ya kuupeperusha muziki wa Tanzania katika masoko ya Kimataifa.
Wataalamu wa masoko wa Kimataifa waliotazama video hiyo katika Youtube, wameshauri kuwa itakuwa jambo la busara kwa Michuzi Media Group, kuihifadhi haki yake katika video hizo, na mameneja wa wasanii au bendi wakae meza moja na menejementi ya Michuzi Media Group, ili wakubaliane kutumia bidhaa hiyo kuwa “demo” ya kuwa-poromote wasanii au bendi zao.
Nashauri:
1.Kuzitumia bila ya ridhaa ya aliyepiga video iwe ni kinyume cha sheria.
2.Kunakili na kubandika (copy & paste) bila ya idhini au ridhaa ya waliopiga video hiyo iwe ni kuvunja sheria na heshima.
Huenda wengi wamestaajabia kiwango cha juu na cha kimataifa katika video hiyo (imepachikwa hapo chini).
Kazi imepeperusha Bongo Kimataifa endelea kwa kasi hiyo hiyo
Anwani ya blogu ya Othman ni: othmanmichuzi.blogspot.com
Hongera nyingi sana sana kwa Othumani Michuzi kutoka kwa wadau wa ughaibuni.
Via:wavuti.com
Add a Comment
Yani amechenkula Eliya atari..... Safi sana kaka!!!
doh huyu nampata vema anapiga picha huku kapiga sarakasi lol big up rafiki yangu Mungu azidi kukupa upendeleo maishani mwako.
Umetisha kamanda, hongera sana
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge